107 views 3 mins 0 comments

KIAMA CHAJA KWA WALE WALIOFUNGA VIMULIMULI VING’ORA NA NAMBA BANDIA

In KITAIFA
February 23, 2024

Na mwandishi wetu DAR ES SALAAM

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kimepiga marufuku wamiliki na madereva wote nchini kutoweka Ving’ora, Vimulimuli, Namba bandia na taa za kuongezwa kwenye magari na pikipiki kama kuna ulazima wa kufanya hivyo basi wanatakiwa kuomba ridhaa ya kupata kibali cha kufanya hivyo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Ameyasema hayo Leo 23,2024 Katika Ukumbi wa makao makuu ya Traffic Jijini Dar es salaam Kamanda wa kikosi Cha usalama Barabarani DCP Ramadhani Ng’azi Amesema king’ora kitafungwa kwenye magari au pikipiki za dharula ambazo zitumikazo Katika misafara ya viongozi, pikipiki za polisi,zimamoto, hospital na pikipiki za kijeshi tena kwa kuzingatia maelekezo ya waziri mwenyewe dhamana ya usalama Barabarani

“Magari na pikipiki yoyote inayotumika Kwa matumizi ya kawaida Hairuhusiwi kufungwa king’ora.ni kinyume Cha sheria Kwa mtu yeyote kufungwa king’ora Katika gari au pikipiki bila kuzingatia utaratibu wa kisheria.wapo baadhi ya wananchi ambao wamegeuza ving’ora kuwa fasheni Katika magari au pikipiki zao.tukumbuke king’ora Cha aina yoyote Katika gari au pikipiki ama ya dharula au la kina maana yake”.Amesema kamanda Ng’azi

Aidha kamanda Ng’azi Amesema kuwa wapo watu binafsi,makampuni au taasisi zinafunga ving’ora Katika magari Yao na kuvitumia bila kuzingatia utaratibu wa kisheria Kwa kufanya hivyo Kwa watu hao

“Makampuni hayo au taasisi hizo zinavunja sheria ya usalama Barabarani na wanastahili adhabu ikiwemo ya kulipa faini ya tozo za kupelekwa mahakamani au vyote Kwa pamoja”. Ameongeza kamanda Ng’azi

Kamanda Ng’azi Amesema jeshi la polisi kikosi Cha usalama Barabarani tutaanza operesheni kabambe ya kukamata magari yote ambayo SI ya dharula na yamefungwa ving’ora na yamefungwa ving’ora bila kuzingatia utaratibu wa kisheria

Hata hivyo Ng’azi Amesema kuwa Kuna baadhi ya watu wanafunga Taa zenye mwanga mkali zinazoongezwa kwenye magari au pikipiki yaani spot light na led bar,wanafunga kama urembo kwenye magari na pikipiki,Kwa kufanya hivyo wanatakiwa wavitoe mara Moja kwani wamefunga kinyume na sheria, utaratibu na kanuni za usalama Barabarani,na jeshi la polisi

Ameongeza pia ni kosa kisheria gari au pikipiki kubandikwa namba bandia zisizo na usajili, ambapo baadhi ya watu wamejenga utamaduni ambao wanajihalalishia kuwa ni sheria kuweka namba bandia kwenye magari, hivyo wanatakiwa watoe mara moja namba hizo kabla ya oparesheni kuanza.

Sambamba na hayo, amesema kunavmagari ambayo yamewekwa taa kutoka kiwandani hizo zinaruhusiwa kisheria mfano magari ya mgodini tu na kwenye mapori wakati wa uwindaji na sivyenginevyo, hivyo anapotoka maeneo hayo aweke kava za kuzuia mwanga mkali barabarani kwani mwanga huo unaweza kusababisha uoni hafifu.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram