148 views 3 mins 0 comments

DUKA JIPYA LA RELAXO KUFUNGULIWA,WAWEKEZAJI WAZIDI KUMIMINIKA

In BIASHARA
February 21, 2024

Kampuni Best Brand Distributor leo wamefungua duka jipya la tatu la viatu vya Relaxo aina zote ‘show room’ mtaa wa Morogoro /Samora ambapo ya kwanza lipo Mlimani Cty na la pili Mtaa wa Nkurumah eneo la kati kati ya jiji Clock Tower.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Best Brand Distributor Khalid Salim amesema kuwa lengo la Kampuni hiyo ni kufungua maduka mengine 20 ifikapo 2025 huku akiahidi kuwa kama soko la bidhaa hizo litakua rafiki wanatarajia kufungua kiwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizo nchini Tanzania.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuwezesha kuwa na mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa maslahi mapana zaidi ya nchi ya Tanzania.

Awali akikata utepe katika duka hilo kama ishara ya uzinduzi wa show room hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amesema Serikali inawahakikishia kuboresha mazingira ya usalama kwa wawekezaji na kuendelea kuwapa ushirikiano ili kusaidia Serikali kutoa ajira za kudumu za muda mfupi kwa wazawa.

Amesema kuwa, Serikali peke yake haiwezi kutoa ajira kwa vijana wote nchini hivyo panapotokea wawekezaji wengi inaleta faraja na mtazamo mzuri kuhakikisha vijana wanaendelea kutafuta vipato vyao kupitia wawekezaji wenye dhamira ya dhati kumsaidia Rais Dkt Samia katika kuhakikisha wanapata fursa nyingi za ajira na viwanda.

“Nitoe pongezi sana kwenu kwa kuisaidia Serikali, kama mnataka kuanzisha kiwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizi niwahakikishie tupo pamoja na nyinyi Serikali imetenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji, mutasaidia kwenye mzunguko wa fedha “amesema Kumbilamoto

Akizungumza katika hafla hiyo Mpoki amesema kuwa show room hizo 20 zitakazofunguliwa lengo ni kuwarahisishia wateja wao kupata huduma zao pembe zote za jiji la Dar es Salaam na zikifuatiwa na show room 2 au 3 kwa mikoa yote ya bara na visiwani.

Salim kikeke ni miongoni mwa wanafamilia wa Relaxo waliofika katika uzinduzi huo  amesema kuwa show room hizo ni mahsusi kwa brand maaruf za viatu Sparx, Flite Telaxo na Bahamas zinazosheheni viatu vya aina mbalimbali vya kutembelea na matumizi mengine.

“Katika show room hizi zina viatu mbalimbali ikiwemo viatu vya mazoezi vya kike na kiume, shule, maabara, hospital madokta na manesi yaani tumesheheni viatu aina zote vya wakati wote kwa mazingira yote ambavyo tunauza jumla na reja reja”amesema Kikeke

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram