148 views 4 mins 0 comments

TANZANIA YAENDELEZA USHIRIKIANO WAO NA MISRI KUPITIA SEKTA YA UCHUKUZI

In BIASHARA, KITAIFA
February 19, 2024

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Uchukuzi leo imekutana jijini Dar es Salaam na Wizara ya Uchukuzi ya Misri lengo ni kuendeleza mashirikiano ya kiuchumi ya sekta ya uchukuzi kati ya nchi hizo mbili na kudumisha mahusiano mazuri yaliopo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa amesema kuwa, mashirikiano hayo yatakuwa na faida kubwa kati Serikali wa Tanzania na Serikali ya Misri pamoja na wananchi wa pande zote mbili.

Amesema kuwa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuipambania  sekta ya miundombinu kwani amekua mstari wa mbele kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya Bandari, Viwanja vya Ndege, Reli pamoja na Barabara.

“Bila ya kuekeza kwenye sekta ya miundombinu katika nchi yoyote hakuna maendeleo ambayo yanaweza kupatikana kwa haraka, sekta hii muhimu sana kwani ndio inayotoa ramani ya uchumi wa nchi hivyo ni vyema Serikali kutoa kipaumbele kwa sekta hii kama alivyofanya Rais wetu Dkt Samia”amesema Prof Mbarawa.

Ameongeza kuwa, Bandari ya Dar es salaaam  ni muhimu sana kwa Tanzania na kiunganishi kizuri kwa nchi ambazo hazina Bandari kama vile Nchi ya Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia pamoja Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Aidha, amesema kuwa lengo la ujio wa viongozi hao mbalimbali kutoka Misri wakiwemo wafanyabiashara ni pamoja na mambo mengine ni kujionea namna nchi ya Tanzania inavyofanya kazi katika Sekta ya uchukuzi pamoja na kujifunza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Hata hivyo, amesema kukamilika kwa mradi wa maboresho wa bandari ya Dar es Salaam (DMGP) kumeifanya bandari hiyo kupata mafanikio makubwa  katika kuhudumia meli na shehena na kuongeza kuwa mpango uliopo sasa ni kuanza ujenzi wa gati 13 hadi 15 ili kuongeza zaidi kasi ya kuhudumia meli na shehena.

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi wa Misri Luteni Jeneral Kamel Alwazeer amesema kuwa, pamoja na mambo mengine wamefika nchini Tanzania kwa lengo kujifunza fursa mbalimbali za kiuchumi kupitia sekta ya uchukuzi kwenye Anga, Reli pamoja na  Bahari.

“Nimekuja na wajumbe mbalimbali pamoja na wafanyabiashara kwa lengo la kujifunza fursa mbalimbali za kibiashara kwa Tanzania kupitia bahari, anga na reli, natamani sana kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kupeana ujuzi”amesema Waziri Luteni Jeneral Kamel.

Ameongeza kuwa, Serikali yake itasimamia uhusiano wa bandari zake na Bandari ya Dar es Salaam hasa katika mafunzo ya kujengeana uwezo kubadilishana uzoefu na matumizi ya Teknolojia ili kuonesha ufanisi.

Aidha, amesema kuwa uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili umeanza tangu Rais wa awamu ya kwanza wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungamo wa Tanzania Hayyat Mwalim Julius Nyerere ambapo amesema ni uhusiano nzuri wa kiuchumi na mashirikiano mazuri hivyo hadi sasa kupitia marais walipo madarakani wamekua wakiendeleza.

Kuna uhusiano nzuri wa marais wetu, tupo tayar kushirikiana nao, tutaleta  bidhaa kama vile nguo, mazulia, mafundi ujenzi pamoja na madawa, pia kuboresha viwanda vya Misri vilivyopo Tanzania na kupeana ujuzi na kupata maslahi kwa nchi zote”amesema Waziri Luteni Jeneral Kamel.

/ Published posts: 1486

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram