208 views 59 secs 0 comments

CHALAMILA:WANANCHI MUJIANDAE KWA KUPANDA KWA BEI YA MAHARAGE

In BIASHARA
February 19, 2024

DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kujiandaa na bei ya juu ya maharage

Akizungumzia suala la sukari katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Februari 19, 2024 katika uwanja wa Msufini Chamazi jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha bei ya maharage pia itapanda.

“Ni kama vile ilivyo mwaka huu wa fedha mwaka huu maharage yatakuwa ghali sana, kwa sababu huko (mashambani) mvua imenyesha kubwa na maharage yameathirika sana, kwa hiyo tujiandae pia kwa bei ya maharage baadaye kwa sababu ya hali ya tabianchi.

Chalamila yupo katika ziara ya mkoa mzima wa Dar es Salaam kukagua kuzindua na kuweka mawe ya msingi ziara ambayo imeanza leo Februari 19, 2024.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram