
Ateta na Papa Francis zaida ya dakika 25,VATICAN
Yapita takribani miaka 25 tangu alipoenda Rais Mstaafu Kikwete
Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu ahudhuria mualiko wa Papa Francis Mjini Vatican,Rais Dkt.Samia katika mualiko amefanya mazungumzo na Papa Francis zaidi ya dakika 25 ikiwa ni katika kuendelea kudumisha demokrasia ya Tanzania Kimataifa.

Katika mazungumzo yao ya faragha yaliyodumu kwa takribani dakika ishirini na tano, wameridhika na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Tanzania; mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu hususan katika sekta ya: elimu, afya na ustawi wa jamii pamoja na changamoto ambazo Tanzania inapitia kwa sasa. Baadaye, wamejielekeza zaidi katika masuala ya kijamii ; masuala ya kikanda na Kimataifa na umuhimu amani.
Wadau mbalimbali wa siasa na kidiplomasia nchini wamempongeza Rais Dkt.Samia kwa kuendelea na udhubutu wa kurejesha mahusiano ya Kimataifa na mataifa ya ushawishi mkubwa wa kidini na kisiasa Duniani.