84 views 45 secs 0 comments

UTALII WA MALIKALE WASHIKA KASI NCHINI WAFARANSA WAFURIKA KILWA KISIWANI

In KITAIFA
February 14, 2024



Kwa miongo kadhaa kumekuwa na dhana ya kwamba wageni wengi wa nje hupendelea zaidi utalii wa kuona wanyamapori, lakini hivi karibuni dhana hiyo imeanza kubadilika kwa kasi ambapo Tanzania imeanza kupokea wageni makundi kwa makundi wakitembelea katika maeneo yetu ya Malikale hususan Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara.

Ni takrikani siku 9 sasa katika kipindi cha Mwezi Februari kuanzia tarehe 03 – 11, 2024, Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA imeweza kushuhudia Meli zilizosheheni makundi ya Watalii kutoka Mataifa mbalimbali zikipishana kutia nanga katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara na kufikisha idadi ya watalii wapatao 445 kwa safari nne (4) za kitalii zilizofanyika.

Kwa mara nyingine Februari 11, 2024 TAWA ilipokea kundi la nne (4) la watalii wapatao 114 kutoka Ufaransa ambao waliingia Kilwa kisiwani kwa ajili ya shughuli za utalii na kufanya idadi ya watalii wa nje waliotembelea hifadhi hiyo ndani ya siku 9 tu kuwa 445.

Hata hivyo, TAWA inategemea kuendelea kupata wageni wengi kutoka Kona mbalimbali za Dunia kuja kutembelea na Kutalii Katika Hifadhi hiyo kongwe yenye utajiri mkubwa wa kihistoria.

Kwanini Kilwa Kisiwani na Songo Mnara? Wahenga walisema ukitaka kuujua uhondo wa ngoma, uingie ucheze, hivyo TAWA inaendelea kuwakaribisha watalii wote wa ndani na nje kutembelea hifadhi hii kujionea yaliyomo.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram