220 views 13 secs 0 comments

HIFADHI YA MAGOFU YA KILWA KISIWANI YAENDELEA KUFURIKA WATALII WA NJE

In KITAIFA
February 14, 2024



Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara inaendelea kupokea makundi makubwa ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali Duniani ambao wanafika nchini mahsusi kwa ajili ya kutembelea hifadhi hiyo iliyosheheni utajiri wa kihistoria na maajabu ya magofu ya kale kwa shughuli za utalii.

Kwa mara nyingine ikiwa ni kundi la tatu la watalii wa nje ya bara la Africa kutembelea hifadhi hiyo katika kipindi cha mwezi Februari pekee, Februari 07, 2024 ilipokea tena watalii wapatao 102 kutoka uingereza wakiwa na meli iitwayo The Hebridean Sky ambapo Kampuni ya kitalii iitwayo Takimis Holidays Ltd iliratibu safari hiyo.

TAWA inaendelea kunufaika na matokeo chanya ya filamu maarufu iitwayo Tanzania The Royal Tour iliyochezwa na muongoza watalii namba moja Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupokea makundi ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali Duniani katika hifadhi zilizo chini ya usimamizi wake.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram