175 views 30 secs 0 comments

MWENEZI MAKONDA AZUNGUMZA NA BARAZA LA WAZEE WA MKOA DAR ES SALAAM

In KITAIFA
January 19, 2024

Na Mwandishi wetu

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda Amewashukuru Baraza la Wazee na Wana CCM wote kwa mchango wao wa maombi ya kumpatia jambo jema ikiwa ni sehemu ya baraka na mafanikio.

Mwenezi Makonda ameyasema hayo leo tarehe 19 Januari, 2023 alipopokelewa katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni.

Akizuzungumza katika Kikao hicho na WanaCCM pamoja na Wazee, Mwenezi Makonda amesema heshima ya CCM inatokana na kutatua kero za Wananchi.

” *Heshima ya Chama chetu ni kutatua changamoto za watu, tumepewa nafasi na ridhaa maana yake tunanayo majibu ya changamoto walizonazo Wananchi wetu* ” Alisema Mwenezi Makonda.

Pia, Amewataka Viongozi na Wananchama kwa ujumla kuimarisha chama (CCM) kuanzia ngazi za Matawi na Kata.

Aidha, Mwenezi Makonda Amebainisha maadhimisho ya CCM yataanza kufanyiwa sherehe kwenye kila Kata na kusema kuwa Wenyeviti wa Kata, Madiwani ndio wenye majukumu ya kuandaa na kila Jumuiya iwe na siku yake ya maadhimisho na lengo ni kuhakikisha maendeleo yote yaliyofanywa kwenye kata yanasemwa ambapo itakuwa chachu ya kuona uhai wa Chama na Jumuiya zetu za Chama Cha Mapinduzi.

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram