172 views 5 mins 0 comments

MRISHO:KWA MWAKA HUU WA FEDHA 2023/24 UNATARAJIA KUHUDUMIA MAKASHA ZAIDI YA MILIONI MOJA NA LAKI 2

In KITAIFA
January 15, 2024

Mkurugenzi wa Bandari, Mrisho Mrisho amesema kwa mwaka huu wa fedha, 2023/24 wanatarajia kuhudumia makasha zaidi ya Milioni Moja na laki mbili.

Alisema kwa mwaka wa fedha 2022/23 Bandari ya Dar es Salaam walihudumia shehena Tani milioni 21.46, na malengo kwa mwaka uliopita ilikuwa ni kuhudumia Tani milioni 19.6 ambapo Tani hizo walizozihudumia walifanikuwa kuvuka lengo.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam wakati akitekeleza agizo la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, (TPA), Plasduce Mbossa la kutembelea maeneo yao ya utendaji kazi kuona hali ya utendaji inavyoendelea na kuthibitisha yale yaliyosemwa na Mkurugenzi huyo siku ya tarehe 9 Januari mwaka huu.

“Tani milioni 21.46 zilihudumiwa mwaka wa fedha uliopita 2022/23 malengo ilikuwa ni kuhudumia Tani milioni 19.6 kwahiyo tulikua tumevuka lengo kwa Tani Milioni 2, ulijinganisha tena kwa mwaka wa fedha uliopita nyuma yake 2021/22 ilikua ni Tani milioni 18 hivyo kituo hiki kimevuka lengo tulilowekewa na tulivuka lengo hata lile ambalo la kiwango Cha shehena iliyohudumiwa 2021/22”



Alisema kwa mwaka huu wa fedha 2023/24 kuanzia mwezi Julai 2023 hadi sasa tayari wamehudumia Tani milioni 12 na malengo waliyowekewa na serikali kwa mwaka mzima ni kuhudumia Tani milioni 22.

“Pamoja na lengo tulilowekewa la kuhudumia Tani Milioni 22 sisi kwa kituo hiki Cha bandari ya Dar es Salaam tumesema lazima tuhudumie Tani milioni 24 hivyo tutavuka lengo zaidi, TPA nzima kwa maana ya Bandari zote kwa mwaka 2022/23 ilihudumia Tani milioni 24, hivyo kwa mwaka huu Tani hizo tutazihudumia sisi pekeetu”

Kadhalika, Mrisho alisema walipita kwenye maeneo maalumu ya utekelezaji, kutembelea eneo la kuhudumia shehena ya magari, ambalo ni maalumu kwaajili ya meli za magari na kwa sasa wana ufanisi mkubwa sana baada ya kupata eneo hilo lenye urefu wa Mita 320



Alisema katika eneo hilo kuna yadi maalumu ya kuhifadhia magari ambapo kwa wakati mmoja tuna uwezo wa kuhifadhia magari 6000 ambapo kwa mwaka katika eneo hilo wanaweza wakahudumia magari yapatayo 250,000 Hadi 300,000 kwa mwaka

“Kwa wakati mmoja unaweza ukawa na meli hata tatu au nne ukazihudumia zikiwa ba maxmam namba ya magaru 6000 unaweza ukazihifadhi katika yadi Ile ambayo inaukubwa wa square Mita 72, 000 na kwa mwaka uliopita tumeweza kuhudumia magari kati ya 250,000 Hadi laki 300, 000 kwa mwaka”

“Eneo hilo Lina mifumo ya ulinzi na usalama na kwa sasa huwezi kusikia Zile kelele za miaka ya nyuma kuhusu usalama wa magari kwenye bandari”



Kwa upande wa eneo la kuhudumia meli za mwambao, Mrisho alisema wanahudumia meli za Zanzibar na Comoro na ni maeneo muhimu kwasababu maeneo hayo bidhaa kama za majumbani, vyakula, vifaa vya ujenzi vinavyotoka dar es salaam kwenda maeneo hayo na vile vinavyotoka kama Zanzibar kuja huku eneo hilo linatumika kwa shughuli hizo ndogo za mwambao.

Pia alisema wao kama Bandari ya Dar es Salaam wanajivunia kuwa sehemu ya wadau waliofacilitate miradi ya kitaifa ikiwemo bwawa la mwalimu Nyerere, mradi wa Bomba la mafuta n.k

Alisema Gati namba 1-4 ni maalumu kwaajili ya kuhudumia meli za mizigo mchanganyiko lakini pia Gati namba 5 – 7 yanatumika kwaajili ya kutumia shehena ya makasha (makontena) yanayoingia na kutoka ambapo eneo la kuhifadhia kontena kwa wakati mmoja wanaweza ukahifadhia kontena 10,000 .



“Maeneo haya yote tunashukuru Mradi wa DMDP matokeo yake ni haya, kupata Gati namba 0 na kuboresha magati kuanzia 1-7, lakini pia uchimbaji wa kina Cha bandari”Alisema Mrisho

Mrisho alisema eneo la Gati namba 8-11 ndilo lililokuwa linatumiwa na mwekezaji aitwae TIPS lakini kwa sasa wanaendelea kusimamia shughuli zote za kuhudumia makasha katika eneo hilo.

Mbali na hayo Mrisho alisema kwa sasa wanaendelea kuongeza matumizi ya Bandari kavu ya kwala ambapo mazungumzo yanaendelea na TRC kuongeza namba za Wagon kwani eneo hilo limeunganishwa noja kwa moja na Reli kutoka Bandari ya Dar es Salaam mpaka Kwala.

Alisema Kuanzia Ijumaa ya tarehe 12 hadi kesho 15 watapokea meli mpya 16 za kontena, mizigo mchanganyiko ambapo ukiunganisha na meli wanazoendelea kuzihudumia wataenda kwenye nafasi ya meli 40 hivyo alisema wataendelea kuongeza uwezo wa kuzihudumia meli hizo.

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram