198 views 56 secs 0 comments

DR MALUGU:TUKO KWA AJILI YA KUISAIDIA SERIKALI LAKINI TUNAMITAJI MIDOGO

In BIASHARA, KITAIFA
January 13, 2024

Mkurugenzi wa kampuni ya biashara ya mitandao Dr Queen Malugu Amesema Kuna watu wengi ambao wanaosoma wapo Kwa ajili ya kuajiliwa lakini yakati hizi ni ngumu sana kuajiliwa lakini wapo Kwa ajili ya kuisaidia serikali kwani Bado tunamitaji midogo

Hayo ameyasema Leo Tarehe 13,2024 Katika Tafrija ambayo walioifanya wafanyabiashara hao pamoja na mkurugenzi wao wa kampuni ya biashara Amesema watu wengine wanajihusisha na mambo mabaya Kwa kukosa ajira



“Lakini Mimi ninawafunza watu ambao wamemaliza vyuo na hawajarudi kwao mikoani lakini wapo dar es salaam hawafanyi vitendo vichafu ila wanafanya biashara ya maendeleo na kuwasaidia familia zao na wameweza Kujenga nyumba huko vijijini kwao”. Amesema Malugu

Aidha Amesema ni vitu vikubwa ambavyo vinavyofanywa na hawana Muda wa kuajiliwa Kwa sababu elimu ni kuongeza akili Katika kichwa chako Ili uweze kuwasaidia jamii Kwa akili ambayo uliyoipata na sio kwamba elimu lazima uwajiliwe unaweza ukawa umejiajili na kupata pesa nyingi na tofauti ungeenda na kumfata mtu akuajili



“Tunawafikia watu wote Kupitia mitandao ya kijamii na Kuna watu live na watu wote munaotuona hapa ni watu ambao tunandugu na ambao ndugu zetu wengine ni watanzania na wengine sio watanzania tunandugu zetu wapo mikoani tunawafikiahia taarifa Kuhusu biashara yetu Kwa kuwapigia Simu Kwa kuwaambia na kikubwa Zaidi tunawafikia Kupitia mitandao ya kijamii”Ameongeza Malugu

Hata hivyo mkurugenzi Malugu ameweza kutoa gari mbili Kwa shindano ambalo aliloliweka Kwa madairekta na wafanyabiashara na mtu atakaeshinda atakabidhiwa gari aina ya rengee na Prado

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram