Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Mamlaka ya dawa ya vifaa tiba TMDA yakanusha juu ya uwepo wa dawa duni ya matoleo ya dawa aina ya fluconazole ya vidonge ya miligramu 200 yaliyotengenezwa na kiwanda Cha universal corporation kilichopo Kikuyu nchini Kenya
Tarehe 29 desemba 2023 TMDA iliweza kupokea taarifa iliyotolewa na taasisi ya udhibiti chakula na dawa nchini Rwanda (Rwanda FDP)
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya dawa ya vifaa tiba TMDA Adam Fimbo Amesema matoleo DUNI ya dawa hiyo imeweza kuisha Muda wake wa matumizi Agosti 2025.
RFDA imependa kufanya hivyo Ili kutekelezwa matakwa ya shirika la Afya Duniani (WHO) ya kutoa taarifa za uwepo wa dawa duni za bandia Ili mamlaka zingine za udhibiti wa dawa Duniani nazo ziweze kuchukua hatua iwapo matoleo husika yatakuwa yamesambazwa.katika nchi zao
Fimbo Amesema TMDA inapenda kuwajulisha umma kuwa haijasajiliwa dawa hiyo ya vidonge (fluconazole 200 mg tablets )badala yake imesajili dawa hiyo ikiwa Katika mfumo wa kapsuli za miligramu 150 na 200 (fluconazole 150mg na 200mg capsule)kutoka kiwanda hicho
Aidha Fimbo anapenda kuwataarifu umma kuwa TMDA haijatoa kibali Cha kuingiza dawa hiyo nchini .hata hivyo Kwa kuwa Kuna uwezekano wa dawa hiyo kuingizwa nchini Kwa njia haramu na mipaka isiyo rasmi, TMDA ilichukua hatua ya kufuatilia Katika soko la nchi yetu na kijiridhisha kuwa matoleo tajwa ya dawa hiyo hayajaingizwa nchini.
Fimbo Amesema mamlaka itaendelea kufanya ufuatiliaji Zaidi wa dawa zilizosajiliwa kutoka kiwanda hicho pamoja na viwanda vingine Kwa lengo la kuendelea kulinda Afya ya jamii.