158 views 4 mins 0 comments

KUSILUKA:WAWEKEZAJI KUPEWA SAPOTI NA SERIKALI ILI KUZIDI KUWEKEZA

In KITAIFA
January 06, 2024

Na Madina Mohammed

*Serikali inajipa umuhimu wa juu sana kwenye swala hili la mafanikio ya hii kongani ya viwanda

-*Mkoa wa pwani ni mkoa wa uwekezaji,Tunaviwanda 1525,120 ni viwanda vikubwa na vengine ni viwanda vya kati na vengine viwanda vidogo sana

-*Serikali ya awamu ya sita ya Mhe rais Samia suluhu Hassan tokea imeingia madarakani imesema kuwa mkoa WA PWANI unakuwa mkoa wa kimkakati na uhahakikisha tunapata nishati ya kutosha


Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt Moses kusiluka amesema kuwa inafurahisha sana Tanzania kunakuwa na kitu kikubwa Cha mfano na hata serikali na wizara mbalimbali na wizara ya mipango na uwekezaji kwa kuwa na kitu ambacho kinasifiwa kwa wananchi Ili kuonesha maendeleo

Hayo ameyasema Leo 05,2024 Katika kikao kazi Cha maendeleo ya viwanda Katika mkoa wa pwani,kwala,
Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt Moses kusiluka amesema serikali itasapoti huu mradi Kwa sababu tunaona mradi huu ni wa kuonesha watu mradi huu unafaida nyingi sana tunaona serikali inafanya kazi nyingi sana Ili kuhakikisha mradi unakuwa na tuwapongeze bw.janson na wekezaji wengine Kwa mradi huu Kwa kuanza Kwa Muda mfupi sana



“Mhe rais yupo makini sana na amenielekeza nije hapa Ili kuja kuona kwamba maelekezo yake yametekelezwa ujio wangu huu ni kuja kutekeleza maagizo ya RAIS”.

“Wakati mwingine huwa najisikia vibaya ukienda nchi nyingine utakuta unanunua shati inaandikwa imetengenezwa Kenya huko carifonia marekani unanunua shati au tishert Kenya”.Amesema

Nae Waziri wa viwanda na biashara Dkt.Ashatu Kijaji Amesema kuwa viwanda Zaidi ya 200 kutakuwa na ajira Zaidi ya laki Moja Ili kuimarisha uchumi wa Taifa letu



Amesema tumetembelea kiwanda Cha vijora na tumeona utengenezaji wa jivora,vijora hivi tukiwa Dubai tunanunua kumbe vinatengenezwa hapa kwala alafu dubai tunanunua Kwa Dola alfu tunavilejesha kuvivaa nyumbani hapa Tanzania

“Zaidi ya Asilimia 90 ya mabinti ambao tuliowaona Katika kile kiwanda Cha kutengeneza nguo wanatoka hapa kwala na waliniambia kabisa kuwa walitembea mitaani kwetu na kuweza kuwachukua wadada kila aliekuwa na cherehani yake nyumbani na kuanza nao hapa na wengine wanakuja wanakuja”. Amesema Kijaji



Aidha Kijaji Amesema tutakapokamilisha viwanda hivi Zaidi yai 200 kutakuwa na ajira Zaidi ya laki Moja na tutawapata Vijana wengi kutoka ndani ya pwani na ndani ya taifa letu Kwa ujumla Ili waweze kupata ajira na waimarishe uchumi wao Moja Moja na uchumi wa taifa letu kwa ujumla

Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa pwani Abdallah Kunenge Amesema kuwa Mkoa wetu ni mkoa wa uwekezaji tunaviwanda na wawekezaji na Zaidi ya viwanda Kwa upande wa viwanda tunaviwanda 1525,120 ni viwanda vikubwa na vengine ni viwanda vya kati na vilivyobakia ni vidogo sana



Ameongeza kuwa Kwa Kipindi alichoingia Mama madarakani mkoa wa pwani umekuwa na viwanda vingi vikubwa 30 Seven half gate ni viwanda ambavyo vimepanda kutoka viwanda vya kati na kuwa viwanda vikubwa

“Tumekubaliana na mkoa wetu Taasisi zote za ndani ya serikali wanapofata utaratibu wa pamoja wa maendeleo wanaripoti Kwa Rc lazima mipango Yao yaendane na mipango ya mkoa kwani uwezi kupanga ukongani bila ya kushauriana na kueka maendeleo”. Amesema kunenge

Hata hivyo Mhe rais Samia suluhu Hassan ameshaeleza kuwa mkoa WA PWANI unakuwa mkoa wa kimkakati tunahakikisha tunapata nishati ya kutosha Kwa maana ya GESI na umeme tunapata miundombinu mizuri Kwa maana barabara pamoja na reli pamoja na maji Kwa haya ni mambo muhimu sana tuna mita Gage ya TRC na tuna stand Gage zote zinapita hapa na unadhani ni sehemu pekee ambayo mita Gage na stand Gage zinakutana Katika bandari KAVU ya pwani

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram