Na Madina Mohammed
Inawezekana ukafikiria kuwa ni jambo la ajabu kunywa mkojo wako kama”vipimo vya kuishi”Katika dharura kama hiyo lakini watu wengi Katika maeneo mbalimbali duniani wanaamini kwamba kunywa mkojo wako Kuna manufaa Kwa maisha ‘ya kiafya’
Lakini je,kuamka asubuhi na mapema na kunywa mkojo wako mwenyewe kunatibu magonjwa?je,kupaka mkojo kwenye mwili na uso huifanya ngozi kuwa laini na yenye afya kama inavyoaminiwa?madaktari wanasema nini Kuhusu hili?
Kelly Oakley,ni mwalimu wa yoga mwenye umri wa miaka 33 anayeishi uingereza,hivi majuzi alifichua kwamba kunywa mkojo wake mwenyewe kumemsaidia kukabiliana na matatizo ya Muda mrefu,Alisema kuwa dawa hii imempa nafuu ya tezi dume na maumivu ya Muda mrefu.
Kelly alilieleza hivi karibuni shirika la habari la Associated press kwamba amekuwa akinywa mkojo wake Kwa miaka miwili iliyopita
“Nilisikia kwamba kunywa mkojo kunaboresha mfumo wako wa Kinga,husaidia kudumisha afya njema,na ni nzuri Kwa ngozi yako”Kelly alisema
Kwa hivyo nilianza kujaribu jaribio langu la kunywa mkojo si kunywa tu mkojo wake kila siku,lakini pia hupaka kwenye ngozi yake,Alisema kuwa dawa hii ilifanya ngozi yake kung’aa Zaidi.
Watu wengi huita dawa hii’Tiba ya mkojo’Dawa hii pia inajulikana kama ‘Urophagia’
Lakufurahisha kwamba,Kelly sio mtu pekee anayedai kufaidika Kwa kunywa mkojo wake mwenyewe,Hivi karibuni kumekuwa na mifano mingi kama hiyo
“Kunywa mkojo wangu mwenyewe kumenisaidia kupunguza nusu ya uzito wangu “Sampson,46 wa Albert,Canada,aliliambia jarida la sun
Hapo awali Alisema kuwa uzito wake ulipungua Hadi kilo 120,jambo ambalo lilikuwa likimsumbua,lakini Sasa tangu ameanza kunywa mkojo wake mwenyewe,uzito wake umerudi kawaida.
“Rafiki yangu Alitumia video akielezea Tiba ya mkojo,baada ya kutazama video hiyo nilikwenda bafuni nikajaza kikombe na mkojo wangu na kunywa ndani ya siku chache nilianza kuona tofauti ndani yangu”.Alieleza