
DODOMA:Na Madina Mohammed
Jeshi la polisi limemkamata mtuhumiwa Lucas Paul Talimo Aliemshambulia mke wake Kwa kumchoma visu 25 sehemu mbalimbali za mwili wake
Tarimo amekamatwa Leo 31,2023 Alfajili na jeshi la polisi akiwa amejificha Katika Kijiji Cha jema kata ya Oldonyo sambu wilaya ya ngorongoro mkoani Arusha akiwa anajiandaa kukimbia na kukimbilia nchi jirani
Hayo ameyasema Msemaji wa jeshi la polisi SACP David Misime Amesema wanawashukuru wananchi wa kata hiyo Kwa ushirikiano mkubwa waliotoa Kwa jeshi la polisi Hadi kufanikisha Kwa kukamatwa Kwa mtuhumiwa huyo
” ingawa baada ya kuona mkono wa serikali unamfikia alikunywa sumu inayotumika kuua wadudu mtuhumiwa amepatiwa huduma ya kwanza yupo vizuri na taratibu za kisheria zinaendelea”Amesema Misime
Jitihada hizo za kumkamata Tarimo ziliaza Tarehe 12,11,2023 ambapo lilipotiwa tukio la kuchomwa kisu Beatrice James minja na hatimae kufaliki Tarehe 27,12,2023 Katika hospital ya KCMC