116 views 3 mins 0 comments

DKT DENNIS MUCHUNGUZI: MHE DKT BITEKO ANATOSHA ATAMALIZA SHIDA YA UMEME

In KITAIFA
December 31, 2023

Kwa kuelekea mwaka mwingine tumebakiwa na siku 1tu ambayo tunamaliza mwaka 2023 na kuingia mwaka mwingine 2024 ni kipekee tumshukuru mwenyezi mungu aweze kutufikisha salama

Kwa mwaka 2023 Kuna mambo mengi ambayo yametokea hatuna budi kuyakumbuka na kujifunza na wapi tulipokosea Ili unapoingia mwaka mwingine tuwe tumejifunza na kuanza tena upya na tusifanye makosa

Serikali yetu Kwa ujumla tumeona mambo mengi ambayo waliyoyafanya baadhi ya miundombinu tumeiona ikizidishwa kuimalishwa na tumpongeze RAIS Samia suluhu Hassan Kwa kuweza kuwekeza kila sekta,Elimu,Uchumi, Miundombinu,nk

Dkt.Dennis Muchunguzi huyu ni mmoja wa uchambuzi wa maswala ya kisiasa ameweza kutuelezea baadhi ya mambo ambayo serikali imeweza kufanya ikiongozwa na RAIS Samia suluhu Hassan,Makamu wa RAIS, Waziri mkuu,Naibu waziri mkuu,nk ameweza kuwashukuru Kwa kiutofauti Kwa majukumu ambayo wameza kuyafanya Kwa mwaka 2023.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Nampongeza RAIS Samia kuwa ndani ya 2023 amefanya mambo mengi sana na makubwa ndani ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tumeshuhudia juhudi zake kubwa za kuleta maendeleo Katika taifa la Tanzania Kwa usimamizi wake kama mkuu wa nchi mwaka 2023 tumeshuhudia akifanya kazi nzuri sana za kutoa huduma za maji,Afya,Elimu,Kilimo,Lishe,Huduma za maendeleo ya jamii na huduma za kipato Kwa watanzania.

“Tunamshukuru Kwa amani ya nchi ambayo imeendelea kudumu Kwa Muungano wetu na mshikamano wetu na kutengamaa Kwa hali za kisiasa Kwa sitofahau Kwa hali za kisiasa zilizokuwepo huko zamani ameendelea kuzimaliza na tunamshukuru ameendelea kutubeba kimataifa na nampongeza mie kibinafsi Kwa kuweza kutunukiwa shahada ya heshima mbili ambazo Moja alipata Nchini India na nyingine amepata Zanzibar”

Ameendelea kutubeba ameshiriki mikutano mingi kitaifa na ya kimataifa akitekeleza kazi zake na wajibu wake kama RAIS wa Muungano wa Tanzania

MAKAMU WA RAIS

Aidha amempongeza Makamu wa RAIS Dkt Philip Mpango Kwa kazi nzuri ambayo anayoitenda ndani ya nchi mpaka nje ya nchi Kwa mujibu wa mkataba wake ambao amepewa na wananchi na amekuwa Katika maeneo mengi Nchini Kwa kutumikia Taifa lake nampongeza sana Mpango Kwa kumsaidia RAIS na anamtakia umri mrefu ma maisha marefu

Hapa mwishoni aliweza kudhuliwa mambo kadhaa ya kifo Kwa baadhi ya mitandao ya kijamii

WAZIRI MKUU

Kassim majaliwa ameweza kufanya kazi nzuri sana na kutekeleza wajibu wake Kwa kutoa hutuba zake Katika mikutano na bungeni na wizara zake na amemwakilisha RAIS na napongeza waziri mkuu

NAIBU WAZIRI MKUU

Doto Biteko nampongeza sana Kwa kuteuliwa sana na anafanya kazi masaa 24 na tumeona kazi zake ambazo anazozifanya hasa Katika ziara yake ambayo aliyoifanya kwenye bwawa la mto rufiji

Amesema swala la umeme analifanya vizuri na analipigania vizuri Katika kuimarisha watanzania wanapata umeme na hadha ya umeme unatoweka na ametutoa wasiwasi Katika swala la umeme,tulipataga shida kidogo ya adha ya umeme kukatika ila tumeona anapambana nalo

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram