174 views 2 mins 0 comments

TRC WAPOKEA VICHWA VITATU VYA TRENI ZA UMEME

In KITAIFA
December 30, 2023

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Shirika la Reli Tanzania TRC Leo limepokea vichwa vipya vitatu vya treni za umeme ambavyo vilivyoundwa na kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya abiria yaliyoundwa na kampuni ya sung shin rolling stock Technology (SSRST) kutoka Nchini Korea kusini.

Aidha serikali Kupitia shirika la reli ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria Kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango Cha kimataifa

Hayo ameyasema Leo 30,2023,Kaimu mkurugenzi mkuu wa TRC Machibya Masanja Amesema shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya sung shin rolling stock Technology SSRST



“Mabehewa matatu yaliyosalia yanatarajiwa kuwasili Nchini Februari,2024,vichwa 13 vilivyobakia vinatarajiwa kuwasili kwa awamu vichwa 6 vitawasili mwezi machi na vichwa 7 vitawasili aprili 2024″Amesema Masanja

Hata hivyo Masanja Amesema TRC itaanza kupokea seti ya kwanza kati ya seti 10 za treni za kisasa (EMU) mwezi machi 2024 na Mwezi Mei itapokea seti 2,na Juni pia itapokea Seti 2 na Julai itapokea seti 2 na Septemba itapokea seti 2 na seti ya mwisho mwezi oktoba 2024.

“Vichwa vimepokelewa, kiutendaji vina mwendokasi wa kilomita 160 Kwa saa,Mabehewa 27 Katika madaraja ya uchumi na biashara,daraja la biashara (business class) ni mabehewa 13,kila behewa Lina uwezo wa kubeba abiria 45 na mabehewa ya daraja la uchumi (Economy class) ni 14,kila behewa Lina uwezo wa kubeba abiria 78 Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kumuezesha abiria kusafiri Kwa amani na salama”. Ameongeza Masanja



Nae mkurugenzi wa bandari ya Dar es salaam TPA Mrisho Seleman Mrisho Amesema bandari sisi kazi yetu ni kuhudumia meli na kuhudumia shehena hili ni tukio maarum la ushushaji wa mabehewa 27 pamoja na vichwa 3.

“Hii meli imeingia juzi tumeanza kazi siku hiyo hiyo Hadi Jana na Leo asubuhi Kuna mabehewa takribani 16 teali yameshashushwa tuna furaha kwasababu ya kuwa sehemu ya kuhudumia shehena za TRC Kwa sababu ni miradi ya kilelezo”Amesema Mrisho

Shirika la Reli Tanzania linaendelea kupokea Kwa awamu vitendea kazi Kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango Cha kimataifa SGR zoezi la majaribio ya vitendea kazi linaendelea Kwa mujibu wa mkataba Ili kuhakikisha vinaendana na mifumo ya miundombinu iliyojengwa Nchini kabla ya kuanza uendeshaji wa ki biashara

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram