184 views 24 secs 0 comments

Vita vya Israel na Gaza: Hamas yaripoti vifo 241 huko Gaza ndani ya saa 24

In KIMATAIFA
December 27, 2023

Wizara ya afya ya Gaza inayosimamiwa na Hamas imesema takribani watu 241 waliuawa katika kipindi cha saa 24 zilizopita, huku operesheni ya kijeshi ya Israel ikiendelea katika eneo hilo.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amevitaja vita hivyo kuwa ni uhalifu mkubwa dhidi ya watu wake.

Mkuu wa jeshi la Israel Herzi Halevi alisema mzozo na Hamas utaendelea kwa “miezi mingi zaidi”. Israel inasema ilipiga zaidi ya maeneo 100 siku ya Jumanne, huku kukiwa na ripoti za operesheni za ardhini zinazokaribia katikati mwa Gaza.

Milipuko mikubwa ilisikika kutoka Ukanda wa Gaza katika eneo la jirani na Israel mapema siku ya Jumatano.

Wizara ya afya ya Gaza imesema watu 382 pia wamejeruhiwa katika muda wa saa 24.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, Wapalestina wasiopungua 20,915 wameuawa , wengi wao wakiwa watoto na wanawake katika zaidi ya wiki 11 za mapigano.

Madai ya pande zinazopigana hayajathibitishwa. Vita vilianza tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kuongoza wimbi la mashambulizi mabaya kwa jamii ndani ya Israel.

Watu wapatao 1,200, hasa raia, waliuawa. Takribani watu 240 walirudishwa Gaza kama mateka, na baadhi yao waliachiliwa baadaye

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram