179 views 2 mins 0 comments

Pentagon: Tulishambulia kwa mabomu maeneo nchini Iraq

In KIMATAIFA
December 26, 2023

Jeshi la Marekani limeshambulia makundi vya wanamgambo yanaoungwa mkono na Iran nchini Iraq, saa chache baada ya wafanyakazi wa Marekani kujeruhiwa katika shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya kambi ya anga ya Marekan.

Mkuu huyo wa ulinzi wa Marekani alisema maeneo matatu yanayotumiwa na Kataib Hezbollah na makundi mengine yalishambuliwa kujibu mashambulizi dhidi ya vikosi vya Marekani nchini Iraq na Syria.

Mashambulizi ya Marekani yalilaaniwa na Iraq kama “kitendo cha wazi cha uadui”.

Marekani imekuwa ikilenga mara kwa mara maeneo yanayohusishwa na makundi ya wapiganaji nchini Iraq na Syria katika miaka ya hivi karibuni.

Iraq imesema mtu mmoja aliuawa na wengine 18 wakiwemo raia wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Marekani.

Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin alisema shambulio hilo, liliidhinishwa na Rais Joe Biden.

Shambulizi la awali la ndege zisizo na rubani, kwenye kambi ya Marekani huko Irbil katika eneo la Kurdistan nchini Iraq, lilijeruhi wanajeshi watatu wa Marekani, mmoja vibaya, msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa la Marekani Adrienne Watson alisema.

Kundi la wanamgambo liitwalo Islamic Resistance in Iraq, lenye uhusiano na Kataib Hezbollah, lilidai kutekeleza shambulio hilo.

Kambi ya anga ya Irbil hapo awali ilikumbwa na mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na wanamgambo wenye uhusiano na Iran.

Kataib Hezbollah, ambayo inafadhiliwa na Iran, imekuwa moja ya makundi mashuhuri yaliyohusika katika mashambulizi dhidi ya kambi za Marekani nchini Iraq.

Marekani ina wanajeshi wapatao 2,500 nchini Iraq kwa mwaliko wa serikali ya Iraq kuzuia kuibuka tena kwa kundi la Islamic State (IS).

Kuna wanajeshi 900 wa kijeshi wa Marekani kaskazini-mashariki mwa Syria, pia wa kukabiliana na IS, ingawa serikali ya Syria inachukulia uwepo kwao kinyume cha sheria.

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram