154 views 7 secs 0 comments

KINANA:AHIMIZA TAASISI ZA KIJAMII KUWEKA MKAZO KATIKA ELIMU YA UFUNDI NA UJASIRIAMALI

In KITAIFA
December 24, 2023

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amezihimiza taasisi za kijamii kuweka mkazo katika elimu ya ufundi na ujasiriamali, ili kupata mwarobaini wa tatizo la ajira na kuzalisha wataalamu wengi zaidi wa fani mbalimbali.

Kinana ameyasema hayo leo, Desemba 24, 2023, jijini Arusha, alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 10 wa Jukwa la Vijana wa Kiislamu Mkoa wa Arusha (JUVIKIBA).

Kinana amesema kuwa, endapo taasisi za kijamii zitajikita kuhamasisha elimu ya amali (ufundi), vijana wengi watapata utaalamu katika fani mbalimbali ambao utawawezesha kujiajiri, kuajiri wenzao na hata kuwa na sifa ya kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ya fani walizozisomea na kujifunza.

Aidha, amewapongeza vijana wa jukwaa hilo kwa kujitoa kupambania elimu ya ujasiriamali na ufundi ambapo amesisitiza kuwa anaamini jitihada hizo zitawalipa matunda mema kwa kujiingizia kipato badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram