> Atoa mrejesho wa Ziara ya Idara ya Uenezi katika Miko ya Kanda ya Ziwa
> Asema zaidi ya Mikoa 25 imefikiwa na Waziri wa Ardhi kwa utatuzi wa Migogoro ya Ardhi, Matokea chanya yaonekana.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametoa mrejesho wa ziara iliyofanywa na Idara ya Uenezi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 21 Disemba, 2023.
“Idara ya Uenezi tulifanya ziara, tulitoa maelekezo ikiwemo kutokana na kero za migogoro ya ardhi na maji na tulielekeza wizara kutatua kero hizo, na Wizara ya Ardhi ilianzisha utamaduni wa kuwa na kliniki za Ardhi na Waziri Jerry alianzia mkoani Dodoma ambapo zaidi ya Wananchi elfu 41 wamepewa hati, Waziri ameshatembelea mikao 25 kutatua migogoro ya ardhi maana yake kazi inafanyika katika kufanya kazi kumuondolea machungu na maumivu mtanzania pasipo kujali chama chake.”
” lakini CCM imemuagiza Waziri wa Ardhi kuhakikisha tunapata mwarobaini wa migogoro ya ardhi ili kero hizi kuisha kabisa na sasa wameanza kutekeleza agiza hili na wanataka kufanya mpango wa sera za ardhi, tayari wamesimamishwa kazi wafanyakazi 15 waliobainika kuzalisha migogoro na Wizara inajipanga kutumia vema mifumo wa Tehama, CCM inatoa pongezi katika hili”
“Mkoani Kagera, Waziri wa Tamisemi Mhe. Mchengerwa tayari amesaini mkataba wa miradi 15 ikiwemo mkoa wa kagera kuhusiana na utatuzi wa Stendi na Masoko”
” Mkoani Geit zaidi Tsh Bilion 6 zishatolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ujenzi wa mradi wa maji Katoro na Geita wenye uwezo wa kubeba kaya zaidi ya elfu 68000 na mradi umefikia zaidi ya asilimia 98% na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu Disemba basi Maji safi na salama yatapatikana kwa wingi na kwa uhakika.”
Aidha, Mwenezi Makonda amebainisha kuwa tayari Waziri wa Ujenzi Mhe. Bashungwa ameshashuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzj wa Daraja la Sukuma lenye urefu wa Mita 70 na barabara unganishi yenye urefu wa Kilomita 2.294 kwa kiwango cha lami.