262 views 2 mins 0 comments

TAASISI YA MTETEZI WA MAMA WASHEHEREKEA SIKU YA KUZALIWA KWA RAIS SAMIA KWA AINA YAKE

In BURUDANI, KITAIFA
December 21, 2023

Taasisi ya Mtetezi wa Mama hii leo imesema kuwa inatarajia kuungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa January 27/2024 kwa namna ya kipekee ikiwemo kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mohammed Chande amesema kazi kubwa ya Taasisi hiyo nikuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Pamoja na hayo wamemtambulisha rasmi msemaji wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama ambaye ni Madebe Lidali ambaye atahudumu kwenye nafasi hiyo kwa mkoa wa Dar es salaam.


Akizungumza mara baadaa ya kutambulishwa kwake Msema Madebe Lidali amesema katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais samia Taasisi yao imeandaa matukio mbalimbali ili kuungana nae ikiwemo kutembelea watoto yatima,kutoa msaada kwa walemavu,wajawazito,wajane na makundi mengine ya wasiojiweza.

Ameongeza kuwa katika Mfululizo wa matukio yao pia watafanya ziara kubwa katika miradi yote iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita Ndani ya Mkoa wa Dar es salaam lengo likiwa ni kuuelezea umma namna ambavyo Serikali yao inafanyakazi kwa vitendo na si maneno.

Nae Afisa Miradi wa Taasisi hiyo Mohammed Sekamba ameaema kuwa siku ya kilele cha Maadhimisho hayo ambayo ni January 27 mwakani watakuwa na matukio ya kuwaleta watu pamoja kupitia Jogging na bonanza la michezo kati ya Bongo movie na Bongo fleva.



Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Mtetezi wa Mama William Frank Chitande amewaomba wadau mbalimbali kuwaunga mkono kwa kushirikiana nao bega kwa bega katika kutekeleza utoaji wa misaada na mambo mengine ili kumuheshimisha Rais Dkt Samia kwa utendaji wake wakazi.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram