177 views 48 secs 0 comments

CCM YAIPONGEZA WIZARA YA KILIMO KWA UZALISHAJI WA TUMBAKU KUPANDA KUTOKA TANI 60,000

In KITAIFA
December 21, 2023



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amesema Chama Cha Mapinduzi kinaipongeza Wizara ya Kilimo chini ya Waziri Bashe kwa kuendelea kusimamia vema na kuonesha Tija kwa wakulima Nchini.

Mwenezi Makonda amesema kulingana na Takwimu, inaonesha kuwa kwa mara ya kwanza uzalishaji wa zao la tumbaku umepanda kutoka Tani 60,000 hadi kufikia Tani 122,000 ambapo jumla ya dola Milioni 283 zimapatikana kutokana na mauzo hayo kiasi ambacho hakijawahi kupatikana tangu kuanza kulima zao la tumbaku.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenezi Makonda amesema hayo yote ni juhuzi za utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na Sera za Kilimo kikamilifu unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pia, Mwenezi Makonda amebainisha kuwa Tanzania imeanzisha Mnada wa Chai ambapo sasa chai yetu itakuwa inauzwa kupitia mnada wetu na kwa wiki chache toka mnada uanishwe tayaru bei ya chai imeendelea kuimarika hivyo amaomba Makampuni ya chai yaendelee kuunga mkono jitihada hizo za Serikali.

Aidha amesema, Serikali kwa kushirikiana na na wadau wa zao la Pamba wameendelea na juhudi za kuhakikisha wanaongeza Tija ya wakulima wa pamba ambapo tayari kwa mwaka huu 2023 wameshanunua matrekta 100 ambayo yatatumiwa na wakulima wa pamba wakati wa kupanda na kuvuna.

/ Published posts: 1494

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram