Naibu waziri wa mambo ya Ndani Dkt Maduhu Rack Kazi Amesema Wahamiaji wenye ujuzi ni chachu nzuri Katika ustawi wa jamii husika hata KatikaTaifa Ambalo walilofikia Kwa wakati huo
Amesema Wahamiaji wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zingiwemo Kwa kubaguliwa kunyanyaswa pamoja na changamoto za hali ya kimaisha Katika usalama wa familia zao kwani wanaitajika kujifunza Katika mambo mapya hasa katika elimu Utamaduni na kuongeza udugu na ushikamano
Ameyasema hayo Leo 18,2023 Katika viwanja vya mashujaa Naibu waziri wa mambo ya Ndani Dkt Maduhu Rack Kazi Amesema nawaasa wananchi kuwa sehemu kutafuta suruhisho la kudumu Kwa wahamaji kwani ni sehemu muhimu kwenye maeneo ya uchumi yakiDunia pamoja tunaweza na hatuna budi kushirikiana Ili kufikia malengo hayo
“Tanzania imekuwa ikipokea wahamaji Kutoka Katika sehemu mbalimbali Wahamiaji hao wakiwa wakiingia nchi Kwa madhuni mbalimbali wangine wakipita njia Kwa Muda mfupi na wengine Kwa Muda mrefu lakini taifa letu likifaidika Kwa kundi la wahamaji ambalo wanaoingia Kwa kufata sheria na utaratibu kanuni na Viongozi waliopo na vilevile Kwa Kupitia sheria hizo tunawapata wawekezaji pamoja na watalii na wanafunzi wakiwa Nchini kwetu”.Amesema Kazi
Ameongeza kuwa baadhi ya Wahamiaji wamekuwa wakikiuka utaratibu baada ya kuingia Nchini na kukiuka utaratibu wa kuishi kundi hili lisilokuwa rasmi lazima liweze kudhibitiwa vizuri Ili kusudi tuendelee kuimarisha amani pamoja na usalama
Nae Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Gerald Joha Amesema Takwimu zinaonesha kwamba Katika kipindi Cha mwezi januali Hadi novemba 30,2023 jumla ya raia wa kigeni wapatao 1,611,773 waliingia Nchini Kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo utalii,MATEMBEZI,masomo na Shughuli nyingine za Muda mfupi
Kwa upande mwingine jumla ya watu 1,468,808 walitoka Nchini na jumla ya watanzania 373,113 walitoka nje ya nchi na watanzania 369,123 walirejea Nchini kutoka nje ya nchi