
DAR ES SALAAM: Na Madina Mohammed
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi na Baraza la usalama Barabarani la Taifa Kwa kushirikiana na jeshi la polisi wameandaa operesheni maarum ya kudhibiti ajali za barabarani Katika maeneo yote ya nchi
Amesema Baraza litaendelea kusimamia Kwa nguvu madereva Ili kuweza kupunguza ajali barabarani Katika maeneo yote ya nchi hususani Katika barabara kuu za mikoani
Ameyasema hayo Leo 13, Disemba 2023 Waziri wa mambo ya Ndani Hamad Masauni Amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua Kali Kwa wale wanaokiuka sheria hizo na amesema kusiwe na msalie mtume au huruma ya aina yoyote Katika kushughulika na madereva wazembe ambao Wanagharimu maisha ya wananchi wa nchi hii
Wanasababisha ulemavu wa wananchi wa nchi hii wanazalisha mayatima,wanazalisha wajane.jeshi kuwa wakali na wachukue hatua haraka
“Ukaguzi Kwa abiria ambao wanaolewa na kusababisha ajali umepungua na kurudi Katika kiwango Cha kawaida Ili tifanikishe Kwa kile kinachowezekana kuzuia madereva ambao wanaotumia vilevi vya aina yoyote huku wakiwa wanaendesha magari”.
Aidha Mhe RAIS Samia ameweza kutoa magari ya polisi 48 ambayo yatahusika Katika dolia ya kuthibiti ajali
Nae Kamanda wa polisi kikosi Cha usalama Barabarani SACP Ramadhan Ng’azi Ameweza kutoa Ripoti ya ajali Vifo na Majeruhi Kwa kipindi Cha kuanzia 01,01,2023 Hadi 12,12,2023
Amesema Jumla ya ajali zilizotokea ni 1,641 ambapo kati ya hizo ajali 1,057 zilisababisha vifo,Ajali 451 zilisababisha Majeruhi na ajali 135 zilisababisha uharibifu wa vyombo vya moto
“Jumla ya Majeruhi ni 2,562 Kwa wanaume ni 1,721 na wanawake ni 841 jumla ya vifo 1,550 Kwa wanawake ni 361 na wanaume ni 1,189″Amesema Ng’azi