173 views 2 mins 0 comments

JESHI LA POLISI LAVURUGA MIKUTANO YA CUF NA KUHATARISHA AMANI HANDENI

In KITAIFA, UCHAMBUZI
December 13, 2023

Chama Cha Wananchi-CUF kikiwa kinaendelea kufanya hadhara Katika ngazi za kata na wilaya Katika maeneo mbalimbali Ili kujiimarisha Katika chaguzi zijazo

Kwa Takribani mwezi mmoja Sasa,Jeshi la polisi limeweza kujiingiza Katika siasa ya kukwamisha mikutano ya hadhara ya chama Cha wananchi CUF hususani kwenye ngome za CUF

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa habari,Uenezi na Mawasiliano ya umma Mohammed Ngulangwa Amesema Mwenyekiti Prof Ibrahim Lipumba aliongea na umma Kupitia vyombo vya habari kufuatia kuvurugwa Kwa mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika buguruni sheli na hatua zote zilifuatwa za kisheria

Amesema mtendaji kata alitoa taarifa Kwa jeshi la polisi ila OCD Buguruni Alitumia nguvu na jeuri inayotokana na michango ya walipa Kodi kuvuruga mkutano huo na kuwakamata viongozi mbalimbali na kuwaweka mahabusu kituo Cha polisi buguruni

“OCD huyo amerudia kuzuia mkutano wa kata ya Buguruni uliopangwa kufanyika Desemba 10, 2023 bila maelezo yoyote”.Amesema Ngulangwa

Ngulangwa Amesema Chama Cha wananchi CUF kiliendelea kufanya hadhara zake na waliamua kufanya hadhara Katika wilaya ya Handeni Tanga Katika viwanja vya Kwa kivesa kata ya chanika na hadhara hiyo haikufanyika Kwa kuzuiwa na polisi.

Ngulangwa Amesema CUF- Chama Cha Wananchi Handeni kimefuata taratibu zote na kwa upande wa Jeshi la Polisi, “barua ilipokelewa Desemba 6, 2023. Zuio lolote lilipaswa kutolewa ndani ya saa 48 tangu kupokelewa kwa barua hiyo, muda ambao ulikamilika kabla ya Desemba 9. Kwa mshangao mkubwa, leo Desemba 12 ndipo Polisi Handeni wanazuia mkutano wa CUF- Chama Cha Wananchi kwa maelezo yasiyoeleweka”.

Hata hivyo Ngulangwa Amesema CUF- Chama Cha Wananchi kimechoshwa na hujuma hiyo inayofanywa na Jeshi la Polisi ambayo athari yake ni kutaka kurudisha kwenye Siasa za uhasama na CHUKI.

“Tulipoongea na Umma wa Watanzania tunaamini Tamko letu lilifika ngazi za juu kwa wahusika wa pande zote mbili- CCM na Jeshi la Polisi. Kujirudia kwa matukio haya ni ishara kwamba CCM na Polisi wameamua kwa makusudi kusababisha maafa kupitia dhulma yao hii na kwa hakika watabeba lawama ya chochote kinachoweza kutokea, kuanzia leo huko Handeni”.

“Hatuwezi kuvumilia tena kuzuiwa kufanya Siasa kuanzia leo.
Tunatoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kutumia busara kutuliza hasira za wenye kudhulumiwa ambazo kwa vyovyote vile zitaleta madhara na kuharibu uelekeo wa nchi yetu Kisiasa”. Ameongeza Ngulangwa

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram