Na Madina Mohammed
Baada ya kupotea Kwa Muda mrefu kidogo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango Amesema yamesemwa mengi sana na wengine wanasema kuwa yeye ni mzuka
Ameyasema hayo Leo Tarehe 10 Desemba 2023 wakati akiwa katika Ibada ya jumapili Katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska kiwanja Cha ndege DODOMA Amesema kunawale ambao munakumbuka wanaosoma biblia na nawakumbusha zaburi ya 118 Aya ya 17 ambayo inasema “sitakufa Bali nitaishi”
“Mukae Kwa amani niko salama nilienda nje ya nchi kufanya shughuli maarum Kwa takribani mwezi mmoja na sijapungua hata kidogo Kwa hiyo ni baadhi ya mitandao wamevumisha uvumi kuwa amekufa”.Amesema Mpango
Mpango ametoa wito Kwa baadhi ya watu ambao wanaotumia mitandao visivyo kwani wanawaumiza watu wengi sana na Kuna wengine waliumizwa na maneno ambayo hayana msingi
“Mitandao ni mizuri ila baadhi ya watu wanaitumia visivyo mumewaona wajukuu zangu hawakuniona mwezi ila waliponiona wamenikimbilia na kunifata tujitahidi sana kutumia mitandao ipasavyo”.Amefafanua Mpango
Hata hivyo Waziri mkuu kassim majaliwa alishasemaga kuwa Makamu wa Rais kuwa yupo salama na ameenda nje kikazi wakati akiwa Katika Maadhimisho ya kitaifa jijini dodoma mwaka huu
“Mhe.philip Mpango Ambae yupo nje ya nchi Kwa majukumu na waachane na ule mtandao ambao unaosema sema mambo ya ajabu ajabu yupo nje Kwa majukumu anawatakia kila la kheri watu wote waliofika Katika Maadhimisho haya ya kitaifa anawaombea sana na kuwatakia kila la kheri”Amesema waziri Majaliwa