NIRC Mbarali, Mbeya
Wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakiendelea na mafunzo kwa vitendo juu ya ukarabati kinga miundombinu ya umwagiliaji kwa viongozi wa wakulima katika skimu za Umwagiliaji za Matebete, Igumbilo Isitu, Gonakuvagogolo pamoja na skimu ya Mwaru zilizopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mafunzo hayo yamehusisha skimu zaidi ya saba zilizopo wilayani humo wataalamu pamoja na wakulima wametembelea katika skimu za umwagiliaji kujifunza kwa vitendo jinsi ya kutambua viashiria vinavyopelekea uharibifu wa miundombinu ya Umwagiliaji.
Mafunzo ya ukarabati kinga miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima yana lengo la kuanzisha mpango wa Umoja wa kujitegemea kwa wakulima katika kuendesha kazi za ukarabati wa kinga, ukaguzi wa miundombinu pamoja na tathimini ya uharibifu na uchakavu ili kuandaa mpango kazi wa ukarabati na utekelezaji.
Kupitia elimu ya ukarabati kinga miundombinu ya umwagiliaji wakulima wataweza. kudhibiti kwa haraka viashiria vya uharibifu mdogo wa miundombinu hali itakayorahisisha kuokoa fedha ambazo zingetumika katika ukarabati mkubwa.Wataalam wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakiendelea na mafunzo kwa vitendo juu ya ukarabati kinga miundombinu ya umwagiliaji kwa viongozi wa wakulima katika skimu za Umwagiliaji za Matebete, Igumbilo Isitu, Gonakuvagogolo pamoja na skimu ya Mwaru zilizopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Mafunzo hayo yamehusisha skimu zaidi ya saba zilizopo wilayani humo wataalamu pamoja na wakulima wametembelea katika skimu za umwagiliaji kujifunza kwa vitendo jinsi ya kutambua viashiria vinavyopelekea uharibifu wa miundombinu ya Umwagiliaji.
Mafunzo ya ukarabati kinga miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima yana lengo la kuanzisha mpango wa Umoja wa kujitegemea kwa wakulima katika kuendesha kazi za ukarabati wa kinga, ukaguzi wa miundombinu pamoja na tathimini ya uharibifu na uchakavu ili kuandaa mpango kazi wa ukarabati na utekelezaji.
Kupitia elimu ya ukarabati kinga miundombinu ya umwagiliaji wakulima wataweza. kudhibiti kwa haraka viashiria vya uharibifu mdogo wa miundombinu hali itakayorahisisha kuokoa fedha ambazo zingetumika katika ukarabati mkubwa.