192 views 2 mins 0 comments

JAI KINONDONI YAFANYA HARAMBEE KUKUSANYA FEDHA KUTOA HUDUMA KWA JAMII.

In KITAIFA
December 07, 2023

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Islaah Islamic Foundation Dkt Alhaji Hassan Sulle ametoa wito kwa Makampuni,Mshirika,Taasisis na Watu wenye Uwezo kuchangia Jumuiya ya Akhlaaqul Islam (JAI) Kinondoni ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa watu wenye uhitaji ikiwemo wagonjwa Mahospitalini.

Wito huo ameutoa Mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam wakati akiongoza kongamano la harambeee ya kukusanya fedha kiasi cha shilingi milioni sitini ambazo zinahitajika kwa ajli ya kutekeleza kazi ambazo JAI imekua ikizifanya kwa jamii yenye uhitaji.

Dkt Sulle amesema kuwa JAI imekua ikifanya kazi kubwa ya kusaidia makundi mbalimbali ikiwemo Watoto wanaoishi katika mazingira magumu,wagonjwa wanaokosa fedha za kupata huduma za matibabu pamoja na kuchangia damu,hivyo inatakiwa kuwezeshwa kifedha ili itekeleze majukumu yake ipasavyo.



“Napenda kutumia fursa hiii kuwaomba watu wenye uwezo wa kifedha,Makampuni ,Taasisi na Mashirika mbalimbali yajitokeze kusaidia Mchango wake katika kuwezesha JAI iweze kua na uwezo wa kidfedha ili itoe huduma inazotoa kwa jamii yenye uhitaji”amesema Dkt Alhaji Sulle

Kwa upande wake Amir wa JAI Kinondoni Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Hamis Mwanga amesema kuwa JAI inatoa huduma mbalimbali ikiwemo kusaidia watoto wanaotelekezwa na wazazi wao,kuchangia damu kwa wagonjwa wenye uhitaji.

“Desemba 31 mwaka huu JAI itafanya zoezi la kuchangia damu katika hospitali ya Mwananyamala ikiwa lengo ni kusaidia watu wanaohitaji damu kuokoa maisha yao wakiwemo wajawazito wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua “amesema Amir Mwanga



Nakuongeza kuwa”kupitia harambee hii tumepata kiasi cha fedha taslimu Milioni sita, laki saba na elfu themanini (6,780,000) lakini kuna fedha zingine zimetolewa kama ahadi hivyo endapo tutazikusanya zote tunatarajia kupata jumla ya kiasi cha shilingi milioni kumi na moja,napenda kuwashukuru wale wote waliojitolea.

Nae katibu wa Afya Hospitali ya Rufaa Mwananyamala Rajab Omari amesema kuwa Hospitali hiyo ina wagonjwa wengi ambao wanahitaji msaada kutokana na kukosa fedha hivyo Jumuiya ya JAI imekua ikitoa mchango mkubwa katika kusaidia wagonjwa hosptitalini hapo

/ Published posts: 1435

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram