238 views 36 secs 0 comments

AWESO AKAGUA APATIKANAJI MAJI HANANG,HUDUMA YA DHARURA YAIMARISHWA

In KITAIFA
December 07, 2023

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) amewahakikisha Wananchi upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya Vijiji na Kata zilizoathiriwa na maporomoko ya matope kutoka Mlima Hanang’ yaliyopelekea miundombinu ya maji kuharibiwa na kusababisha madhara ikiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Waziri Aweso ameeleza hayo leo tarehe 06 Disemba 2023 akizunguka katika maeneo hayo na kujionea hali ya upatikanaji huduma ya maji na jitihada ya kurejesha Miundombinu ya Maji katika mji wa Katesh na maeneo mengine

Amesema Wizara ya Maji imechukua hatua ya dharura kwa kuweka matenki ya maji 30 yaliyosambazwa katika makambi, vitu vya huduma za afya na maeneo ya vijiji vyote yaliyoathirika hasa Kata za Gendabi, Jorodom, Ganana, Katesh ,Mogitu na Dumbeta

Aidha, Waziri Aweso amekabidhi Matenki ya maji 30 ya lita 5,000 kwa Madiwani na kuhakikisha yanaletwa Maboza ya Maji matano yanayopeleka maji katika matenki na kuwafikishia wananchi huduma ya majisafi na salama muda Wote.

Waziri Aweso amekagua na kujionea mitambo ya kuchimba kisima cha maji ambayo tayari imeanza kazi ambapo itasaidia kuongeza maji katika vyanzo ambavyo havijaaribiwa na maafa hayo.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amtembelea maeneo ya wahanga na maeneo ya wananchi wanaopata huduma ya maji na kukabidhi bomba zenye urefu wa mita 2880.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram