269 views 3 mins 0 comments

WIZARA YA AFYA NA BARAZA LA TIBA ASILI NIMLI NA TAASISI YA DAWA ASILIA LIMEOMBWA KUONGEZA VIFAA TIBA

In KITAIFA
December 05, 2023

Wizara ya afya na Baraza la Tiba Asili Nimli na Taasisi ya utafiti dawa ASILIA limeombwa kuongeza nguvu Katika vifaa TIba Ili kufanya tafiti za TIba Kwa kina

Hayo yamesemwa Leo 04,2023 Mkurugenzi mkuu wa Islaam Islamic foundation Alhaj Dkt.Sule Amesema Tanzania tunahuwaba wa kufanyia tafiti Kwa wakati mwingine huduma za Tiba Asili zipo Chini ya wizara ya afya na baraza.la Tiba Asili na Tiba mbadala lazima tukubali kuwa nchi zinazoendelea zimekuwa na vifaa Tiba vichache sana vya kufanyia utafiti

“Mara nyingi wizara zimekuwa na kanuni za kutafiti dawa Kwa makundi na ndomana nyuma huko tulikuwa tunatumia korokwini na dawa hiyo ilikuwa nzuri kwa ajili ya malaria lakini Baraza lilipoamua kufanya tafiti wa uwezo wake kutibu kiwango Gani wangapi waweze kupona na wanangapi hawawezi kupona na manake ikaonekana dawa Ile Haina uwezo mkubwa wa kutibu kwetu sisi malaria ikaonekana kuwa sugu wakaitoa Katika mfumo wa Tiba Kwa sababu haikidhi haja Kwa watu wengi”.Amesema Dkt sule

Aidha Dkt.Sule Amesema mtu mwingine anaweza fanya jaribio la kumpa mtu dawa akapona au kufanya kitu kikatokea labda Kwa mtu mmoja au wawili anataka kujiaminisha kwamba Kwa Asilimia 100 amefanikiwa kuondoa tatizo.

DKT.Sule amewaomba wizara ya afya Kupitia Baraza la Tiba Asili Nimli kule na Taasisi ya utafiti dawa asilia na mambo kadhalika ni vizuri Sasa kuongeza nguvu Kwa upande wa vifaa Tiba Ili kufanya tafiti za Tiba Kwa kina na kuweza kuitumia mimea asili Katika kutoa matokeo Chaya ya matibabu Katika jamii

“Lazima tukubali sehemu kubwa ya matibabu yanayotumika duniani malighafi yanayotokana na nchi za afrika tulichokosa afrika ni tafiti za kina na vifaa Tiba vya kutosha Katika tafiti ndio pengine zinatufanya tuwe nyuma lakini naimani zitaendelea kufanyiwa kazi na siku si nyingi tutaweza kujikuta Katika hatua nzuri za utafiti na matokea Bora za utafiti zitakazofanywa juu ya mimea asilia ya maradhi au matatizo mbalimbali ambayo yatakayoweza kutatuliwa na changamoto zake Kutokana na mimea asili na Tiba ambayo imesheheni kuwa nayo Katika Bara la afrika ukilinganisha na nchi za ulaya ambayo sehemu kubwa wanamisitu ya kupanda na sisi tuna misitu ya Asili”Ameongeza Dkt sule

Hata hivyo Dkt.Sule.amesema yapo baadhi ya magonjwa lazima mtu upime na yapo magonjwa mengine hayana ulazima wa kupima Kwa sababu magonjwa yamegawanyika Katika makundi

Aidha ameweza kusema kuwa Tanzania na Kenya wameandaa kongamano la Mdahalo la kiimani Kwa kutengeneza ujirani mwema na kuwapa elimu wasikilizaji wao na pia kufanya maombi Katika mataifa hayo yote mawili na kuwaombea Viongozi wote

Mdahalo huo ukiongozwa na mkurugenzi mkuu wa Islaam Islamic foundation Alhaj Dkt.sule na mchungaji ndacha kutokea Kenya Mdahalo huo umeandaliwa Kwa mambo mawili kuwapa elimu wasikilizaji wao na kuombea Taifa Kwa ujumla Kwa mataifa yote mawili Mdahalo huo utakuwa Kwa siku mbili ya tarehe 16 na 17

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram