Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan , ametoea maelekezo yafuatayo.
1 Amuelekeza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuwa Serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.
2 Majeruhi wote wapatiwe matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali huku Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiendelea kutoa Msaada wa dharura na Uokoaji.
3 Amemuelekeza Mkuu wa Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha Wananchi wote ambao Makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwaajili ya kuwastiri Wananchi hao.
4 Aelekeza tathiminj ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na Taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.