185 views 49 secs 0 comments

KINANA:AWAHAKIKISHIA WANANCHI HANANG KUWA MAELEKEZO YA RAIS DKT.SAMIA YATATEKELEZWA

In KITAIFA
December 04, 2023

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, amewahakikishia wananchi Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara hususani waliokumbwa na janga la mafuriko, kwamba maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, yatatekelezwa kikamilifu.

Cde. Kinana ameyasema hayo leo tarehe 4 Desemba, 2023 alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya Vijiji vya Wilaya ya Hanang.

Aidha, Cde. Kinana amewatembelea na kuwafariji wananchi waliopoteza ndugu zao na waliojeruhiwa na kulazwa hopitalini kutokana na janga hilo ambapo amewapa pole na kuwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.


/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram