225 views 38 secs 0 comments

CCM YATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA MAFURIKO YALIYOTOKEA HANANG MKOANI MANYARA

In KITAIFA
December 04, 2023


> Mwenezi Makonda awasihi Wananchi kufuata maelekezo ya Serikali.

> Awaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa ili mvua kuwa sehemu ya Baraka

” Wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi wanaungana na Mwenyekiti wetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoa pole kwa ndugu zetu wa Mkoa wa Manyara na haswa Wilaya ya Hanang kutokana na janga kubwa tulilolipata la msiba wa Watanzania wenzetu, Hakika ni wakati wa Majonzi na huzuni kubwa kwa ndugu zetu hawa waliokuwa na maisha yao kawaida na kufanya shughuli zao za kujikwamua kiuchumi katika Makazi halali lakini kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko imepelekea baadhi yao kupoteza Maisha ” Mwenezi Makonda.

Pia, Mwenezi Makonda ametoa rai kwa kusisitizia katika Maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema maelekezo hayo si tu kupunguza machungu na maumivu waliyonayo Wananchi wa Hanang bali kuokoa na kulinda maisha yao kwa kadri iwezekanvyo.

Aidha, Mwenezi Makonda amewasihi Wananchi wote wanaoishi maeneo ya milima hususani katika kipindi hiki kigumu kuendelea kusikiliza maelekezo ya Serikali kwa kushuka milimani na kukaa kwenye kambi maalum ambayo imeshaandaliwa na Serikali chini ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram