Kanisa la Spirit Word Ministry lililofungiwa usajili Kwa sababu ya kutuhumiwa kusapoti maswala ya ushoga na serikali kulifungia kanisa hilo Mnamo Mwezi WA 3,2023 na serikali kusimamisha huduma na kufunga ukumbi waliokuwa wanafanyia huduma
Awali serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Kwa kushirikiana na polisi limeweza kumfutia tuhuma hizo baada ya polisi kujilidhisha na uchunguzi waliofanya na kukuta Hana hatia na hakuna ukweli Kwa tuhuma hizo kuwa amefanya
Hayo yamesemwa Leo Novemba 29,2023, Mchungaji mkuu wa kanisa la Spirit Word Ministry Caesar masisi Amesema jambo hili halikuwa zuri sana Katika jamii unapoekewa lebo mtu Ambae ulikuwa unaeshimika kwenye jamii alfu ghafra unapewa lebo ya kuwa wewe ni boss
“Nilizungumzwa mpaka kwenye bunge kanisa langu lilizungumzwa mpaka bungeni na pia Katika mikusanyiko mbalimbali mikubwa walilizungumzia kanisa langu na mimi nikiwa kama kiongozi mkuu nimekuwa lebo kama boss ninaeongoza maswala hayo ya kuhamasisha hakuna yoyote atakaenipenda Kwahiyo hiyo ilikuwa chuki Katika jamii”.
“Ndugu zangu wengi hawakunielewa jamii yote hawakunielewa pia Katika swala la kiroho wale waliokuwa wanajengeka kiroho Katika huduma Katika kanisa langu na ukija Katika kanisa langu wengi ni Vijana Katika Asilimia 98 ni Vijana na wengi niliokuwa nimewakusanya ni wale wakabaji wavuta bangi niliwakusanya Ili wapate huduma na nimepata hasara kubwa sana wale Vijana wamepotea wamerudi kuwa wakabaji na kuvuta bangi”.Amesema Masisi
Aidha masisi Ametoa wito amewaasa jamii wawe makini Kwa kile wanachokisema wanaotumia sosho media Kwa upana wa kutazama jambo,neno Moja unaweza kulisema na kuleta madhara makubwa amezuru kanisa limefungwa na watu waliokuwa kanisani wamepoteza wamerudi nyuma
Na serikali wanapoona vijikripu hivyo vimekatwa wachukue hatua ya kutafakari lile jambo Kwa kumuita muhusika kumuhoji na kutazama lile jambo Kwa upana wake na baadae kulichukulia maamuzi
Hata hivyo masisi Amesema Kwa yule Ambae ameweza kulifanya jambo hilo ni mtu Ambae alikuwa anamfahamu ila amefaliki dunia na hawezi kumshtaki na amemuachia mungu
MADINA MOHAMMED