390 views 2 mins 0 comments

TAASISI YA JAI KUANDAA KONGAMANO KUWASAIDIA WAGONJWA WASIOJIWEZA

In KITAIFA
November 28, 2023

Taasisi ya Jai ni Taasisi ya kujitolea ambayo inayowasaidia wagonjwa wasiokuwa na ndugu na wale wasioweza kumudu gharama za matibabu Katika hospital ya Rufaa Mkoa Mwananyamala wilaya ya Kinondoni.

Taasisi hiyo ya Jai imeandaa kongamano na ndani yake kutakuwa na harambee ambalo kusudio kubwa ni kuchangia na kuwasaidia waitaji ambao ni wagonjwa wasiojiweza ambao kipato chao kinakuwa kidogo kuliko matumizi

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo jumanne 28,2023,Amiry wa Jai wilaya ya Kinondoni Khamisi Omary Mmanga Amesema Tarehe 3 siku ya jumapili kuazia Saa 2 mpaka saa 9 kutakuwa na funlaizi ambayo itakayofanyikia global karibu na veta

Aidha Amesema Katika kongamano hilo.mgeni rasmi atakuwa Makamu wa kwanza wa RAIS wa Zanzibar Othuman Masudi Othuman, Mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa na shekhe wa mkoa.wa Dar es salaam na viongozi wengine

“Haya yote ni kuona namna Gani tunaweza kufanya jitihada za makusudi Ili jamii ya Leo iweze kusaidiwa Kuna mambo mengi ila kusudio kubwa ni kumwangalia mgonjwa Ambae anaitaji mahitaji makubwa na ni vipi tutamsaidia mgonjwa na kuisaidia jamii”

“Juhudi hizo mpaka sasa ni miaka 14 na wazo hilo lilianzia hapa hapa wananyamala hospital kundi la waislam liliguswa na tukaona kufanya uhitaji wa kuwasaidia wagonjwa na tunashirikiana na ustawi wa jamii”. Amesema Mmanga

Vilevile Mmanga Amesema Kuna changamoto nyingi ambazo wanakutana nazo za Asilimia za mapato kinachopatikana ni kichache kuliko mahitaji juu ya wagonjwa, wagonjwa wanaongezeka siku Hadi siku,na serikali Katika idara ya afya bajeti yake ni kubwa na Bado haijitoshelezi

Mmanga Ametoa wito Kwa jamii wajitokeze Kwa wingi na Ili waingie kwenye funlaizi hiyo pamoja na lunch wameeka tiketi ambazo kutakuwa na kiingilio kutakuwa na tiketi ya sh.30000,VIP 50000 na VVIP 100000 na lunch hiyo imeandaliwa Kwa dini zote wanaombwa wajitokeze na kuweza kushirikiana kusaidia

Nae Katibu Mtendaji wa Jai Nassoro Juma Amesema Taasisi hiyo ya Jai huwa inakawaida ya kuchangia damu mara 4 Kwa mwaka,mwezi 8.taasisi.ya Jai ilichangia damu na kuweza kupata yuniti 460 Katika vituo mbalimbali vya Jai

Na anawahimiza wananchi kujitokeza Kwa wingi mwisho wa mwezi wa kumi na mbili Katika uchangiaji damu kwani damu hiyo inawasaidia wakina mama wajawazito na wagonjwa wa sikoseli na kuokoa maisha ya wagonjwa

Madina Mohammed

/ Published posts: 1494

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram