192 views 2 mins 0 comments

LIPUMBA ACHAFUKWA,HATUITAJI KURUDI KATIKA SIASA ZA MAPAMBANO

In KITAIFA
November 26, 2023

Chama Cha Wananchi CUF kimelaani vikali Kwa kuvunjiwa mkutano wao ambao ulikuwa unafanyika Katika viwanja vya buguruni sheli na polisi kuwakamata viongozi 7 bila ya kuwa na kibali maarum

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa chama Cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba Amesema amehuzunishwa na kitendo hicho Kwa kukamatwa Kwa viongozi na kuperekwa kituo Cha polisi Cha buguruni

Lipumba Amesema Jana novemba 24,2023 chama Cha Wananchi CUF wilaya ya ilala kilipanga mkutano wa hadhara viwanja vya buguruni sheli na viongozi wa chama na wazee walifata taratibu za mkutano huo ndani ya siku saba Kwa kutoa taarifa Katika JESHI LA polisi na Kwa Mtendaji kata

Prof. Ibrahim Lipumba amesema kitendo hicho si cha kiungwana licha ya wao kufuata taratibu zote zinazotakiwa kisheria.

Aidha amesema viongozi na wanachama waliokamatwa ni Saba ambapo licha ya viongozi kuonana na OCD wa kituo hicho alionyesha kutoonyesha ushirikiano huku akiwajibu kwa jeuri.

Aidha ameishauri serikali kupitia uongozi wa Rais Samia kutambua kwamba huku chini kuna watu wenye mpango wa kuzuia falsafa ya maridhiano ya kisiasa yaliyofanywa na Rais.

โ€œHatuhitaji waturudishe kwenye siasa ya mapambano sisi tunataka siasa za maridhiano ambazo hata Rais Samia mwenyewe anatangaza siasa za maridhiano, ni ishauri serikali ifanye utaratibu wa kutoa mafunzo kuelezea siasa za maridhiano ni nini?โ€ Amesema Prof.Lipumba.

Hata hivyo amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kuomba radhi kwa tukio lililofanywa na OCD wa Buguruni licha ya viongozi kufuata taratibu zote wakati maandalizi ya mkutano yakiendelea Polisi wanaenda kuvunja mkutano huo jambo ambalo sio jema.

โ€œTunajipanga kwenda kwenye uchaguzi hivyo vitendo kama hivi havikubaliki ukizingatia tupo Dar es Salaam palipofanyika maridhiano sasa sijui huko mikoani kutakuwaje?โ€Ameongeza Prof.Lipumba.

Sambamba na hayo amesisitiza ufanyaji wa siasa za hoja sio malumbano pamoja na Vyombo vya dola kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa na nchi

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram