
Waziri mkuu kassim majaliwa Leo amezindua mradi wa umeme wa REA vijijini na vitongoji Katika mkoa wa songwe
Waziri ameyasema hayo wakati akiwa Katika ziara yake ambayo inayoendelea Katika mkoa wa songwe na ameyazungumza hayo akiwa Katika Kijiji Cha Udugura Amesema jukumu Moja sisi wasaidizi Mhe.Rais Samia ametupa ni kuhakikisha kila mtanzania anaishi kwenye nyumba yenye umeme
Na agizo hili ametupa kwetu pamoja na watu wa REA wapeleke wakandarasi mpaka vijijini wapeleke nguzo na nyaya ziwakalibie wananchi na kila mwananchi avute umeme
Na Mhe.Rais Samia Amesema tunapopeleka umeme tusiangalie nyumba aina ya nyumba iwe ya gorofa weka umeme,iwe ya udongo weka umeme,iwe ya nyasi weka umeme
Aidha Amesema na anataka kusikia wananchi wa vijijini wanaeka umeme Kwa Bei nafuu ni Ile Ile aliyoingia nayo madarakani na kuitangaza ya sh.Elfu 27000
“tumekuja kuzindua umeme uzinduzi wa Leo ni uzinduzi kuashiria kazi ya kupeleka umeme vijijini na vitongoji unaendelea”.
“MENEJA wa Tanesco nilimwambia awaambie na amewaambia kuwa tuna umeme wa aina mbili wale Wenye nyumba ya vyumba viwili sio lazima kuvuta umeme wa nyaya kunateknolojia nyingine ya kimtambo ambacho ukikipachika ndani unakiwasha na kinawaka nyumba nzima”Amesema majaliwa
Hata hivyo majaliwa Amesema serikali ya mama Samia inaringa kwamba tutapeleka umeme Kwa kila mtanzania hata kama umejenga mlimani teknolojia hii ya kubandika kimtambo ni sh.elfu 36000 unapata kimtambo na unawasha nyumba yote hata kama umejenga nyumba ya vyumba kumi tutakufata huko huko
“wananchi kwenye swala la umeme musiwe na shaka tunaringa barani afrika kuwa ni nchi ya pili kusambaza umeme mpaka vijijini kote”, Amesisitiza majaliwa
MADINA MOHAMMED