122 views 2 mins 0 comments

MAJALIWA:SERIKALI YA SAMIA YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU ZAIDI YA BILIONI 579 ZIMEKUJA SONGWE

In KITAIFA
November 24, 2023

Ikiwa ni ziara yake ya pili waziri majaliwa mpaka Sasa na akiendelea kutembelea mkoa wa songwe akitembelea vijiji vitongoji na Halmashauri zake na kutembelea miradi mbalimbali na akizindua miradi ya Ruwasa,shule, hospital

Waziri majaliwa Amesema ziara yangu ni maarumu Kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayojengwa Katika maeneo ya wananchi

“Miradi hii ambayo Dkt.Samia Suluhu Hassan ameamua itekelezwe kwenye maeneo yenu na hasa ni Ile ambayo nyie kila siku huwa munaigusa huwa munaitumia ndio ambayo Sasa tunaipa nguvu Zaidi Ili kurahisisha mwenendo wa maisha ya kila siku “. Amesema majaliwa

Aidha majaliwa Amesema Mh.Rais. Samia anania njema na anatamani watanzania kuendelea kuishi kwenye maisha rahisi Zaidi na amefanya maboresho maeneno haya na ndio anatoa pesa nyingi ikiwemo na barabara

Amesema Barabara hizi zipo kwenye madaraja mbalimbali zipo barabara zinazoonganisha vijiji na vijiji na kata na kata na wilaya na wilaya

Pia Majaliwa Amesema Barabara hizi zinaudumiwa na chombo ambacho Mhe.Rais amekiunda ambacho kinaitwa TARURA ndo wanashughulikia barabara na ndani ya wilaya

“unapotaka kuunganisha wilaya na wilaya mkoa na mkoa lakini taifa letu na mataifa ya jirani wanashughulikia Tantroad na mkoa huu wanashughulikia hao Tantroad”.

“wananchi tokea Jana nilipokuwa ireje nimeona mambo mengi makubwa sana kwenye taifa hili yanayofanyika nilipita ireje mara ya mwisho 2018 na ireje niliyoiona Jana sio ireje niliyoiona 2018 kunamabadiliko makubwa sana mambo mengi yamefanyika changamoto nyingi zimeendelea kutatuliwa na kazi hiyo inaendelea”. Ameongeza majaliwa

Majaliwa Amesema jukumu letu sisi wasaidizi Mimi na mawaziri wezangu,Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya,ni kuhakikisha tunasimamia miradi hii inakamilika

“nimeeenda kuona mradi mkubwa sana wa maji mradi huu ndio mkakati mkubwa wa maji wa kupeleka maji kwenye maeneo ya wananchi tunajua tunamaeneo mengi na yatasemwa”, Amesisitiza majaliwa

Zaidi ya bilioni 579 zimekuja mkoa wa SONGWE na zimeenda Momba, zimeenda Ireje,Mbozi na Halmashauri zake zote

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram