418 views 54 secs 0 comments

BISHANGA:MKOA WA SONGWE NI LANGO KUU LA SADC

In KITAIFA
November 24, 2023

Mkoa wa Songwe ni mkoa mpya ambao umeanzishwa mwaka 2016 lakini jumla ya mtandao Km 1073.32, Km 256 zote ni za lami lakini Km 816 ni barabara za Mkoa,ni za changarawe”

Akizungumza na wananchi Katika ziara ya waziri mkuu mkoani songwe Meneja wa wakala wa barabara Tanzania Mhandisi Suleiman Bishanga Amesema Mkoa wa Songwe Kwa hali ya barabara kwa sasa ziko vizuri na zinapitika bila shida kwa maana ya kwamba kwa Wilaya zetu zote ambazo zinahusisha majimbo ya Ileje, Mbozi, Vwawa, Momba, Songwe na Tunduma, kwa majimbo yote haya yanapitika bila shida

“Mtandao wetu wa Barabara tunaupata kwa kutengeneza bajeti ambayo tunatengewa na serikali, jumla ya Bajeti kwa mwaka huu wa fedha tuna jumla ya Bilioni 9 kwa upande wa matengenzo na Bilioni 2.6 kwa upande wa Maendeleo”

“Tuna miradi ya kimkakati kama mkoa, tuna miradi ambayo imeainishwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi na Wizara kupitia Mtendaji mkuu, wametuhusisha na wametuelekeza tuweze kutengeneza barabara zipitike na kuondoa changamoto kwa wananchi”Amesema Bishanga

Aidha Bishanga Amesema Barabara ambazo ni za kimkakati kwa mkoa wa Songwe ni barabara ya TANZAM ambayo watu wanapitia kwenda Zambia na SADC, kwa maana hiyo mkoa wa songwe ni lango kuu la SADC

Vilevile Tuna barabara ya lami ambayo inatoka Tunduma kuelekea Katavi kwenda Kigoma hadi Manyovu kwa maana ya kuelekea Burundi, barabara hizi kwetu kwa mkoa ni muhimu kwasababu Zina magari mengi lakini Zinaongeza kiuchumi mkoa lakini kwa Taifa kwa ujumla

/ Published posts: 1903

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram