220 views 2 mins 0 comments

MWAKIPOSA: UONGOZI HAUJI KAMA UPEPO UONGOZI NI MAANDALIZI

In KITAIFA
November 23, 2023

Chama Cha mapinduzi ccm kimeweza kuwasajili wanachama wake 130 ambao ni wanafunzi wa Chuo Cha st.joseph na st.maria na wamepata kuelewa Itikadi ya Chama cha mapinduzi.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa serikali ya mtaa dovya lazaros mwakiposa amesema kati ya wanafuzi hawa Kuna viongozi ndani Yao wa badae lakini uongozi hauji kama upepo uongozi ni maandalizi

“Chama Cha mapinduzi kitu ambacho kimefanikiwa mpaka Leo duniani kote na wanakishangaa wanajua kuwapika viongozi na ukiona mpaka kiongozi anadiliki kugombea ujue huyo amepikwa,ametengenezwa amenyooka ndomana ameruhusiwa kuingia mtaani agombee”Amesema mwakiposa

Mwakiposa Amesema Chama hiki kina walimu,walezi,washauri,na kina watu wanaokuongoza Ili uwe kiongozi bola lazima upitie ngazi Kwa ngazi

Hata hivyo mwakiposa amewasisitizia wanafunzi wao wa Uvccm hao kuwa na uvumilivu,kikao ndio uhai wa mwanachama na kikao ndo kila kitu na chama Cha mapinduzi ndicho kinawapa mikopo na wakithamini.chama hicho

Nae Mwenyekiti wa Vijana Seneti ya vyuo na vyuo vikuu Othuman salimini amesema kama mwenyekiti ataendelea kusimamia Ilani ya chama Cha mapinduzi na kuhakikisha Dola 2024 tunasimama kikamilifu na 2025 tunamtetea Mh.rais Samia kuchukua mitano mingine

“Wasomi vyuo st Joseph na Santa Maria,tutamlinda na kumchagua Dr Samia suluhu Hassan”Amesema salimini

Pia tunamshukuru Mh.Rais.samia Suluhu Hassan Kwa kutujali wasomi Kwa kutupa mikopo mpaka Sasa Asilimia 73 wasomi wamepata mikopo st Joseph na Asilimia 23 nyingine iliyobakia wanaimani na serikali Kupitia IDARA ya vyuo na vyuo vikuu mkopo uliobakia utaendelea kutolewa

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram