360 views 3 mins 0 comments

MAJALIWA:AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA WAKUU WA IDARA WAKASIKILIZE KERO ZA WANANCHI

In KITAIFA
November 23, 2023

Waziri mkuu kassim Majaliwa Leo Alhamis 23,2023 ametembelea Hospital ya rufaa iliyopo mkoa wa songwe ambayo imeendelea kujengwa na imeshaanza kutumika na viwango vyake vinarizisha

Waziri mkuu kassim Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuleta fedha kwa utaratibu ili majengo yakamilike.

Hospital hiyo Bado inaendelea na ujenzi na Jengo la magonjwa ya dharura , maabara na jengo jipya,majengo hayo bado yanaendelea kujengwa na bado yataendelea kujengwa

“Nimeanza ziara Leo kwa kuja kuona Hospitali yetu ya rufaa mkoa wa Songwe ambayo imeendelea kujengwa na nimepita huko ndani imeanza kutumika lakini viwango vyake pia vinarizisha”

“Mkoa huu wa Mbozi unakwenda kwa Kasi sana na lazima muendelee kujipanga vizuri, na serikali yenu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inawaunga mkono, na kwasababu Rais anawaletea fedha nyingi ambapo mpaka sasa mkoa huu zimeshaingia zaidi ya Bilioni 579 kwaajili ya miradi mbalimbali” Amesema Majaliwa

Aidha Majaliwa Amesema Hospitali hiyo inayojengwa hapa mkoani Songwe ni ya kimkakati, mkoa huo unapakana na nchi jirani ya Zambia na Malawi, ambao wapo ndugu zetu wa Zambia na Malawi hawana huduma kubwa kama inayotolewa hapa, maana yake na wao watakuja hapa mbozi kutibiwa, kwahiyo hapa tuna utalii wa kimatibabu

“Mganga mkuu umeletwa hapa uhakikishe huduma za afya kwenye mkoa huu zinaimarika, Si tu hospitali hii ya Mkoa na hospitali za makao makuu ya Wilaya zote, Hospitali Makao makuu ya Halmashauri zote, vituo vya Afya vyote, na zahanati zote, kila mahali huduma lazima iende vizuri”

“Hapa tulipata tatizo tulipoanza kuleta vifaa baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu wakawa na tamaa na hivyo vitu na mmoja tukamkamata akiwa anaiba kifaa muhimu sana cha kupima magonjwa ya wakina mama ya ndani ya tumbo, alikua anakiiba akauze, na sasa tumefanya mabadiliko ya mganga mkuu”

“Wananchi, serikali yenu ipo imara, Rais wetu ambaye ametupa malengo ya nini tufanye kuwahudumia nyie malengo yake bado yapo palepale kwa kuwahudumia nyie, na amesisitiza sana kwamba huduma mnazitakiwa kuzipata ni Yale maeneo yote ambayo ukiamia tu unaanza kuyagusa ikiwemo elimu, Afya, Maji, kuimarisha Barabara na Kilimo”Amesisitiza majaliwa

Hata hivyo amewataka Wakuu wa Wilaya,waende kwa wananchi vijijini wakawasikilize matatizo yao, wayaratibu, tuwahudumie, na serikali hii imejidhatiti kwaajili ya kuwatumikia wananchi, hivyo iteni mikutano ya kero nendeni na wakuu wa idara sikilizeni kero zao

/ Published posts: 1886

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram