
Wakala wa majengo TBA imesema kuwa mpaka Sasa jumla ya fedha wanaowadai wapangaji wao ni Zaidi ya sh.bilion 7.8 ambazo zinazodaiwa Kwa wapangaji wake zikiwemo taasisi za umma.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo Jumatano 22,2023 Mtendaji mkuu wa wakala wa majengo TBA Daud kondoro jambo hili limekuwa kikwanzo kwenye juhudi zetu za kutekeleza mipango yetu ya maendeleo Kwa ukarabati wa nyumba zilizopo pamoja na Kujenga nyumba mpya ambazo zitaweza kupangishwa na kuuzwa Kwa watumishi wa umma
“Mpaka Sasa tunakabiliwa na changamoto ya uhaba wa nyumba bola za makazi mpaka kufikia oktoba 31 2023 TBA inadai Zaidi ya billion 7.8 za Kodi ya pango kutoka Kwa wapangaji wa nyumba ambapo Zaidi ya billion 3.5 ni madeni ya taasisi mbalimbali za serikali”Amesema Kondoro
Aidha Amesema TBA imeazimia kuchukua hatua Kali za kisheria Dhidi ya wapangaji wote wanaodaiwa Moja ya hatua zitakazochukuliwa ni kuwaondoa wadaiwa sugu kwa nguvu kwa kutumia dalali wa mahakama ambao ndio wamepewa.zabuni kwa niaba ya TBA
“Kwa Sasa tayari kampuni ya udalali wa mahakama iitwayo WINS Auction Mart imeshakabidhiwa orodha ya wadaiwa wote Kwa ajili ya Utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa na zoezi hili litaendeshwa nchi nzima kuanzia tarehe 1 Desemba 2023”. Ameongeza Kondoro
Katika hatua nyingine Amesema Kondoro Kwa hatua nyingine itakayofuata ni kuwaondoa kwenye nyumba na kuwafungulia kesi za madai mahakamani na wadaiwa hao watakao kuwa wameondolewa Ili kuhakikisha wanalipa madeni hayo licha ya kuwa wameshaondolewa kwenye nyumba




Madina Mohammed