124 views 3 secs 0 comments

DKT BITEKO AKAGUA MAJENGO YA WIZARA YA NISHATI,SERA,URATIBU NA BUNGE MJI WA SERIKALI-MTUMBA

In KITAIFA
November 22, 2023


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko aliambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jimmy Yonaz, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu pamoja na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo mbili.

Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dkt. Biteko ameshuhudia ujenzi ukiendelea ambapo kwa sasa umefikia asilimia 69 na Mkandarasi anayehusika na ujenzi huo ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na Mkandarasi ni SUMA JKT.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram