136 views 7 secs 0 comments

WAZIRI DKT GWAJIMA NA JUMUIYA YA WANAWAKE TANZANIA UWT KUENDELEZA AFUA ZA USAWA WA KIJINSIA NA KUPAMBANA NA UKATILI

In KITAIFA
November 21, 2023


DODOMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum *Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wamejadili kuimarisha ushirikiano kwenye ajenda za kuendelea kumkomboa Mwanamke Kiuchumi, kiongozi, kijamii na kupambana na ukatili wa kijinsia.

Akizungumza na Katibu Mkuu wa UWT Ndugu Jokate Mwegelo Ofisi za Makao Makuu Jijini Dodoma 21 Novemba, 2023 Dkt. Gwajima amesema wameweza kujadiliana juu ya mipango mbalimbali ya kisekta inayohusu kumkomboa mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwa ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na kuendelea kuhakikisha Wanawake wanainuliwa kiuchumi ikiwa ni dhamira thabiti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kujenga na kuimarisha jamii iliyo bora na rafiki kwa Watoto na Wanawake wote Nchini.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram