138 views 2 mins 0 comments

JESHI LA POLISI NCHINI LIMEPOKEA MAGARI 43 KUTOKA KAMPUNI YA ASHOK LEYLAND

In KITAIFA
November 21, 2023



Jeshi la Polisi Nchini leo Novemba 21, 2023 limepokea magari 43 kutoka Kampuni ya Ashok Leyland ikiwa ni jitihada za Serikali kuliwezeshwa Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Akiongea katika hafla iliyofanyika bwalo la maafisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema magari hayo yametokana na mkataba wa masharti nafuu wa mwaka 2013 kati ya Serikali ya Tanzania na India ambapo ulikuwa na jumla ya magari 881 na baadhi ya magari mengine yalishawasili nchini na kusalia magari mia mbili, “tupo katika hatu za mwisho kupokea magari yaliyosalia ambapo leo tumepokea magari 43. Mhe. Sagini alisema

Katika hatua nyingine Mhe. Sagini amelitaka Jeshi la Polisi kutenga bajeti za matengenezo ya mara kwa mara ya magari hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu. Aidha pia amewataka wawakilishi wa Kampuni ya Ashok Leyland na mdau wake Kifaru Motors kuhakikisha upatikanaji wa msaada wa kiufundi na vipuri pale itakapohitajika.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu Jeshi la Polisi Nchi, Kamishna wa Polisi Menejimenti ya Rasilimali watu, CP. Suzan Kaganda amesema magari hayo yatatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuliwezesha Jeshi la Polisi katika maboresho yanayoendelea ili kuongeza ufanisi wa kutoa huduma kwa wakati kwa wananchi.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa India Nchini Mr. Manoj Varma amesema ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na India ni wamuda mrefu ambapo makabidhiano ya magari kutoka kampuni ya Ashok Leyland italisaidia Jeshi la Polisi kutimiza majukumu yake kwa urahisi na kwa wakati.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram