269 views 9 mins 0 comments

MBUNGE WA JIMBO LA ULANGA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA RUBY INTERNATIONAL LTD AMETOA HAMASA KWA WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

In KITAIFA
November 10, 2023

MBUNGE wa Jimbo la Ulanga na Mkurugenzi wa kampuni ya Ruby International limited inayojishughhulisha na uchimbaji pamoja na ununuzi wa madini ya vito (SIPNEL)Tanzania na nje ya nlchi Salim Hasham Amesema wanaendelea kufanya shughuli hizo ikiwa lengo kubwa ni kupata riziki na kusaidia nchi Kwa ajili ya kusapoti kauli mbiu ya Vision  2030 madini ni maisha na utajiri.

Pia Amesema wanajaribu kuwatia hamasa na wengine ambao hawapo kwenye sekta  hiyo ili waweze kuingie  Kwaajili ya kwenda kufanya kazi hiyo ili kupata riziki napia Kuitangaza nchi na kuipatia mapato hivyo kazi hiyo wameanza muda mrefu kwenye migodi ya spinel miaka kama kumi iliyopita.

Hasham  amameyasema hayo Nevemba 8 jijini dodoma katika mahojiano maalumu na waandishi wa Habari waliotaka kujua namna alivyowekeza kwenye madini ya vito kule wilayani Ulanga ndani ya mkoa wa Morogoro.

Hasham Amesema kuwa uchimbaji wa madini aina ya spinel haukuanza hivi karibuni bali ameianza Yeye akiwa mdogo sana wakati huo maeneo hayo ambayo hivi Sasa wanachimba huko nyuma walikuwa wanatembea Kwa miguu kuelekea kwenye makazi ya watu.

“Spinel haijaanza Leo ni vile tu watu walikuwa hawajuwi kwamba Kuna madini yanaitwa spinel hivi Sasa  yameingia sokoni na yanaonekana kama mahitaji yake ni makubwa na uchimbaji wake ni mgumu kidogo na hata upatikanaji wake sio rahisi na gharama za uendeshaji ni kubwa pia na madini hayo yanagharama kubwa zaidi kuliko mengine lakini haina maana kwamba kuliko madini yote yanayochimbwa hapa nchini “,amesema.


Nakuongeza kuwa “ukilinganisha na madini ya Tanzanite ,madini ya aina ya spinel yanazidi thamani kwahiyo tunafanya kazi kumsaidia Rais DKT.Samia lakini pia tunawafamisha na vijana wetu ambao wengine walikuwa hawaelewi na unajua madini yamekuwepo tangu mimi nikiwa mdogo na hadi leo nina mvi hivyo tunawafundisha na wengine Ili waweze kuja kuifanya hii kazi Kwakuwaofa zaidi na kutimiza malengo ya Serikali na kuipatia kipato nchi yetu .”Amesema Mbunge Hasham

Akizungumzia uwepo wake nchini Thailand Kwa ajili ya soko la madini hayo ya vito Mbunge Hasham Amesema  madini ya spinel hitaji lake ni kubwa Duniani na soko lake pia na madini hayo yanachimbwa kwenye nchi tatu, Tanzanaia ,Bama, na vetnam lakini wazalishaji wakubwa ni Tanzania hivyo mwitikio ni mkubwa lakini madini yaliyopo hayatoshelezi kwenye soko la Dunia na ameshiriki maonyesho mengi huko nje na lengo kubwa lilikuwa ni kuhakikisha madini yanapanda thamani na sio kuwa local kwani gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa zaidi.

Akotolea mfano upande wa mafuta Kwa Kwa mwakajana walikuwa wananunua sh 2300 kwa lita ila Leo mafuta yanakwenda mpaka sh 3500 hivyo hatuwezi Kila siku unauza madini ya gram Moja Kwa sh. Milioni Moja wakati mafuta yamepanda manaake Hawawezi kuendelea kufanya kazi hiyo hivyo lazima wapandishe thamani ya madini hayo.

Kuhusu tafiti za kisayansi kwenye madini ya spinel

Mbunge Hasham Amesema kuwa jambo  kubwa Kwa serikali kupitia sekta zote za kimkakati Kwa maana mawasiliano ,nishti ,majini wanatakiwa kujua anaposimama Waziri pale Bungeni na kusema kwamba wanachangia Pato la Taifa Kwa asilimia kadhaa manaake wanafanya kazi kubwa na ndio wachangiaji wenyewe kwahiyo uwepo wa mawasiliano kwenye hiyo sekta ni muhimu kwani wakipata mawasiliano hawatapa shida ya uagizaji wa vitu

Amesema wakipata umeme wakutosha hawatakuwa na shida ya kununua vitu vingine Kwa sababu umeme uatakuwepo lakini wakipata barabara nzuri pia zitarahisha baadhi ya mambo kwenda vizuri.

“Pale mgodini mimi ninawatu 800 au zaidi ya 800 Sasa angalia mfano mtu akijikata inabidi kuwasha gari kumpeleka hospitali ya Wilaya  karibu kilometa 11 hadi 12 kwenda na kurudi unaweza kuona ni kilometa ngapi hivyo kama Serikali inaweza kurahisisha kwenye maeneo hayo basi wao watazalisha Kwa wingi na Serikali kupata zaidi .”Amesema .

Nakuongeza kuwa” changamoto ambayo ameiona kwenye upande wa Serikali Wizara hazina mawasiliano mfano Wizara ya madini kazi yake ni kutafuta wawekezaji  ili kuwekeza na wakishapata mwekezaji inampeleka eneo kama Ulanga  na ukimpeleka pale anamuacha hafu hawajui kama ataishije je barabara itamfaa au haitamufaha ili kupitisha vitu vyaka Kwa haraka hizi ni changamoto “amesisitiza .

Ameongeza kuwa kwenye eneo la hospitali pia hakuna hospitali nzuri watu wanakuja kuwekeza ajira za kudumu zinakuwa si chini ya  1000 na zile za  kawaida pia zinabeba watu wengi zaidi ya 3000  hao watu unawasaidia vipi kuhusu hospitali na Yeye kama Mbunge wanahangika ili kuweza kupata  hospitali Sasa wale watu wakiumia wanakwenda kutibiwa wapi kwahiyo mambo kama hayo hivyo Wizara lazima ziwe na mawasialiano .

Amesema Yeye kama Mbunge amezungumza sana juu ya Serikali kufanyia kazi changamoto hizo jampo kukatika Kwa umeme nijambo la kitaifa lakini ataendelea kusema na Imani ni kwamba Rais DKT. Samia ni msikivu hivyo wataendelea kujipanga vya kutosha ili watanzania wapate umeme utakaoweza kuhudumia watanzania wote.

Akimzungumzia Rais DKT. Samia kuhusu mwelekeo wa nchi kupitia sekta ya madini 2030 Amesema Kwanza anampongeza Rais kwani royal tour imeweza kutangaza sekta hiyo Kwa kiasi chake japo Kuna mahala  inawezekana watendaji wa Wizara hawakumweka wazi kwasababu Kuna baadhi ya madini wanaitangaza Tanzanite zaidi kwenye utalii na wameacha madini mengine .

“Kama mmenifuatilia vizuri mwakajana nilitangaza suala la mining tourism kama mlifika mgodini kipindi naanza kujenga kale kanyumba lengo lilikuwa nikuitambulisha mining tourism Tanzania kwahiyo tunajipanga vizuri lengo ni kumsaidia Rais hivyo nampongeza kwani royal tour imezaa matunda na DKT.Doto Biteko amefanya kazi nzuri na ndio maana unaona Leo yuko pale kwani ameitendea haki Kwa kiasi chake alipokuwa Waziri lakini unamuona Anthony Mavunde na bahati nzuri pia tumepata Waziri kijana msikivu .

Amesema kuwa kutokana na hilo wanaouwezo wa kufikisha maoni yao na anakwenda kuyafanyia kazi na wameshaaza kujadiliana na ukizingatia ni kijana mwenzao hivyo wanasikilizana vizuri na kwasababu wao wapo site hivyo ukichanganya na utalaamu wa watalaamu basi kunaweza kutokea kitu kizuri zaidi hivyo mama DKT. Samia wanamuhaidi Kwa kushirikiana na mawaziri wake watahakikisha wanamsaidia ili kusogenza sekta hiyo ili ifike pale panahitajika.

“Nitoe rai Kwa watendaji wa Wizara ya madini pamoja na Waziri na watu wa maliasili tushirikiane kwasababu hizi sekta ziwe kitu kimoja hivyo mhe Rais amefanya kazi yake sahihi na nadhan ameona  jambo Kwa mhe. Mavunde  na ndio maana yuko pale lakini nimepongeze katibu wa Wizara naye yuko vizuri sana hivyo nawashauri waendelee kupambana kuhakikusha sekta inafika mbali sana na Mimi naendelea Kuitangaza na kuhakikisha madini yanapanda Bei

Kuhusu Jimbo la Ulanga Amesema Yeye sio mzoefu sana kwenye siasa lakini naweza kusema Ulanga kulikuwa hakuna watu wanaijua lakini kwasasa ukitaja Ulanga ,mahenge watu wanajua ulanga ni nini hivyo wanejitahidi kuisogeza Ulanga  na hata Serikali sio kwamba wanajua maeneo yote na Ulanga kwenye miaka mitatu ijayo watu watakuwa wanakuja zaidi kwasababu Kuna miradi mkubwa mitatu inakwenda kuanza ya uchimbaji madini hivyo miaka mitatu ijayo itakuwa sio hii ya Leo .

Pia Amesema Kwa upande wake alishasema kwamba atatumia rasilimali zake na atashauri Serikali kuhakikisha kwamba anasaidia kwenye eneo alikotoka kama Mbunge ikiwemo kurudisha hisani yake kama Mbunge hivyo Kuna mambo mengi ambayo ameyafanya .

Amesema kuwa hivi  wameshapata pesa Kwa ajili ya kuanza kujenga hospitali ya Wilaya na eneo tayari lipo ilakwasasa hivi wananchi wa Ulanga wanategemea hospitali ya ifakara pia alinunua la wagonjwa lenye thamani zaidi ya sh. Milioni 120,000 Kwa ajili ya wananchi kwenda hospitali bila kujari,alitoa matrecta Kwa ajili kulimia.

ameongeza kuwa amepata hospitali ya Wilaya ,majengo mapya ,barabara ya lami kutoka ifakara kwenda hadi songea lengo ni  kuufungua mkoa wa Morogoro na mlimba kwenda Njombe na ulanga kwenda liwale .

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram