146 views 41 secs 0 comments

ROBERTINHO WAMUONDOA SIMBA WAMREJESHA MATOLA

In MICHEZO
November 07, 2023


Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robertinho) pamoja na kusitisha mkataba wa Kocha wa Viungo Corneille Hategekimana

Simba imesema katika kipindi cha mpito kikosi kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Selemani Matola huku mchakato wa kutafuta kocha mpya ukiendelea

Uongozi wa klabu ya Simba inawashukukuru makocha hao Kwa mchango wao ndani ya klabu ya Simba na inawatakia kila la kheri Katika majukumu Yao mapya

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram