231 views 45 secs 0 comments

ROBERTINHO:NAIPONGEZA YANGA KUSHINDA DERBY

In MICHEZO
November 05, 2023


Akizungumza baada ya timu yake kufungwa magoli 5-1 katika mchezo dhidi ya Yanga, Kocha wa Simba, Roberto Oliveira “Robertinho” amesema kipindi cha pili wachezaji wake walipoteza umakini na ndio maana wakaruhusu magoli mengi

Amesema “Magoli mawili tuliyofungwa kipindi cha pili wachezaji wetu (Simba) walizubaa na kupoteza umakini, walifikiri kuna faulo wenzetu wakaendelea kucheza na wakafunga. Nawapongeza wapinzani wetu (Yanga) kwa kushinda Derby (Dabi) na sisi tumepoteza mchezo muhimu.”

Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Simba msimu huu katika Ligi Kuu Bara, pia ni cha kwanza kwa Robertinho akicheza dhidi ya Yanga

/ Published posts: 1205

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram