226 views 3 mins 0 comments

HUDUMA ZA MAWASILIANO KIKWAZO KWA WACHIMBAJI WA MADINI YA SIPNEL

In KITAIFA
November 02, 2023

SERIKALI imeombwa kupeleka huduma ya mawasiliano ya simu za kiganjani katika kijiji cha Epanko Halmashauri ya Mji Mahenge wilaya ya ulanga Mkoani Morogoro ili kurahisha mawasiliano katika uendeshaji shughuli za uchimbaji madini ya vito (Spinel) katika kijiji hicho.

Mbali na hilo pia imeombwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika katika maeneo ya migodi hili kuweza kusaidia kutozalisha kwa hasara kama ilivyo sasa.

Akizungumza wa waandishi wa habari wakati walipotembelea mgodi wa Franone Mining and Gems wanaozalisha madini ya Spinel kwa lengo lakupata elimu kuhusu madini hayo Meneja Mgodi Elias Thomas amesema kuwa wamekuwa na changamoto ya mtandao wa simu za mkononi ambapo mtandao unaopatikana ni mmoja tu ambao pia unapatikana kwa shida.

Thomas amesema huduma ya mawasiliano ya simu za kiganjani ni muhimu hususani maeneo ya migodini kutokana asili ya kazi zao hivyo ni muhimu kwa Serikali kulipatia kipaumbele.

Aidha Thomas amesema kupitia uzalishaji wa madini ya Spinel wameweza kurudisha kile wanachokipata kwa jamii kwakujenga nyumba sita kwa wananchi waliokuwa na uhitaji ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya barabara na kujenga vyumba vya madarasa.

Akizungumzia kuhusu kukatika katika kwa umeme hasa katika maeneo ya migodi amesema hali hiyo inachangia kuendesha uzalishaji kwa hasara hata Serikali pia kukosa mapato ambapo amaiomba Serikali kuhakikisha maeneo yote ya migodi kuwa na umeme wa uhakika.


“Mgodi umetoa ajira kwa vijana zaidi ya 200 ambao ni wazawa na siyo wazawa lakini pia tumekuwa tumechangia uchumi wa nchi kwakuwa waaminifu katika ulipaji wa kodi na tunaihaidi Serikali kuendelea kulipa kodi kwa uaminifu pia kuchangia maendeleo ya maeneo yanayotuzunguka ambapo tunachimba aya madini. “amesema Thomas,.

Kwa upande wake Semeni Bakari ambae ni mama lishe katika mgodi huo ameipongeza Serikali ya muungano wa Tanzania kupitia Rais wa awamu ya sita DKT. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema uwepo wa mgodi umesaidia kuwepo kwa miundo mbinu mizuri hasa upande wa barabara ambapo kwa sasa zinapitika muda wote.

Amesema anamshukuru pia mkuwekezaji mzawa ndugu Onesimo Mbise kwa kuwekeza katika eneo hilo kwakuwa wameweza kujipatia ajira na wanaendesha maisha yao bila shaka yoyote na wanaendelea kuimarika kiuchumi.

Huku Jesse Mtui ambae ni mfanyakazi wa mgodi huo amesema kupitia mgodi huo ameweza kupata ajira ambayo inamsaidia katika kuendesha maisha yake.

Ameongeza kuwa kwa kukosekana mawasiliano ya simu za kiganjani yeye kama kijana inampa wakati mgumu kwa kuwa yuko mbali na familia yake hivyo anakosa kuwasiliana nao kwa wakati.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram