130 views 2 mins 0 comments

JOKATE MWEGELO:AHIMIZA WAZAZI KUWA NA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO

In KITAIFA
October 27, 2023

Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania Chini ya Mwenyekiti wa UWT Mary Chatanda imeridhishwa na Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo Katika mikoa ya Tanzania Bara mara baada ya kufanya ziara zake za Kupitia na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo ijumaa 27 2023 Katika ofisi ndogo za chama Cha mapinduzi ccm lumumba Katibu mkuu wa UWT Jokate Mwegelo Amesema ziara hiyo aliongoza mwenyekiti wa UWT Mary Chatanda na Zainabu khamis pamoja na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM na kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la UWT iliyoanza Tarehe 3.24 julai Katika mikoa ya njombe,Lindi, Mtwara na Ruvuma

Mwegelo Amesema kamati ya Utekelezaji imeendelea kuhimiza wanawake na wananchi Kwa ujumla walionufaika na mikopo ya asilimia 10 ya fedha zilizotengwa na Halmashauri za wilaya kuirejesha Kwa wakati Ili kutoa fursa kwa walengwa wengine

Aidha amewahimiza wazazi kuwajibika Katika malezi Bora Kwa watoto Ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili hususani suala la ukatili kwa wanawake na watoto ambayo imekuwa changamoto Katika jamii zetu

“ziara hizo zimeleta mafanikio makubwa sana Kwa jumuiya ya wanawake Tanzania UWT Kwa kuongeza wanachama wapya 514,032 Kwa ujumla ya mikutano ya hadhara 737 ambayo imefanyika kwenye kata 750, wilaya 62 na miladi 1,284 imekaguliwa Katika mikoa 10 iliyofikiwa”. Amesema mwegelo

Hata hivyo Mwegelo Amesema kamati ya Utekelezaji ya UWT inapongeza hatua za serikali ya awamu ya sita Kwa kusaini mikataba ya uendeshaji na uwekezaji wa bandari Kwa kuamini ni yenye tija na italeta matokeo makubwa ya kukua Katika sekta ya kuichumi,kijamii na kibiashara

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Chini ya Rais DKT.Hussen Mwinyi kuendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 Katika kuelekea kufikisha maika mitatu madarakani ambapo sherehe hizo zinatarajia kufanyika siku ya tarehe 4 oktoba 2023 visiwani Zanzibar

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram